“Msalaba ni wimbo unaohusu na kueleza juu uzito wa Msalaba unaomgusa mtu aliyetambua msalaba kuwa ndio Suluhisho la maisha yake, Pale ambapo unapitia hali flani unakosa
msaada basi unaamua kumgeukia mwenye Msalaba na kumwambia Nainua macho yangu nitazame Msalaba wako hapo ndipo penye haki niliposafishwa Dhambi zangu zote.” – alisema Fanta
Hii ni video mpya kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Julius Fanta, Video ikiwa imeongozwa na director Joachim kutoka Blessing Studio, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Tyros Music chini mikono ya prodyuza Elias & Mo.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika kuwa itakubariki kila wakati, Amen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Julius Fanta kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 743 155 268
Facebook: Fanta Julius
Instagram: @fantajulius
Youtube: Julius Fanta
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni