Breaking

Jumatano, 20 Mei 2020

Somo :- Lijue Taifa La Israel Kiroho Uliombee Upate Baraka


Mwalimu : Mtumishi Joseph Elisa (PhD Cand)

 Shalom Wapendwa!!

Lengo la somo
- kuifahamu kibibilia  Israel
- kuweka Mzigo Ndani yako uweze kuliombea Taifa la ISRAEL

Taifa la Israel kibibilia limetokana na kabila 12 ambazo ni Uzao  wa mzee Yakobo. Watoto hao wa Yakobo ni hawa wafuatao, (Rubeni, Simon, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni Hawa ni watoto wa mke mkubwa wa Yakobo Lea) 

Yusufu na Benjamen ( Hawa ni watoto wa Mke mdogo wa Yakobo Aitwaye Raheli), Daniel na Naftali ( Hawa ni watoto wa suria mjakazi wa Leah aitwaye Bilha Bilha aliyezaa na Yakobo), Asheri na Gadi ( Hawa ni watoto wa Yakobo aliyezaa na mjakazi wa mke wake Raheli aitwaye Zilpa)
Kumbuka Yusufu hakutengeneza kabila 12 za Taifa la ISRAEL kwa sababu alikuwa Uhamishoni Misri lakini Baadaye Baba yake Yakobo aliwabariki watoto wake Yusufu ( wajukuu ) wakatengeneza Taifa la ISRAEL. Watoto wa Yusufu waliotengeneza taifa la ISRAEL kwa uzao wao ni Manase na Efraimu.

Kwanini Tunaiombea ISRAEL na kuibeba kiroho ?
Zaburi 122:6-7 Utakieni  Yerusalemu(ISRAEL) amani na wafanikiwe wakupendao, Amani ikae ndani ya kuta zao na kufanikiwa katika majumba yao
Isaya 62:6-7 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako Ee Yerusalemu,hawatanyamaza mchana wala usiku, ninyi wenye kumkumbusha Bwana msiwe na kimya wala msimwache akae kimya mpaka atakapoifanya imara Yerusalem na kuwa sifa kuu Duniani
Mpendwa mtu wa MUNGU kumbuka ukiliombea Taifa la ISRAEL unapata baraka,
Kumbuka ISRAEL ni LANGO
Kutoka 4:22 Nawe umwambie Farao Bwana asema hivi Israel ni mwanangu mimi mzaliwa wa kwanza wangu, mpeni Ruhusa aende akanitumikia
Hapa tunaona wazi Taifa la ISRAEL ni Mzaliwa wa Kwanza, hata Jina la ISRAEL ni jina la Yakobo ambaye uzao wake ndio umetengeneza kabila 12 za Taifa teule la ISRAEL. Kama ISRAEL ni mzaliwa wa kwanza wa MUNGU ni lango la kupitishia Baraka zetu
Tambua Ukiibariki ISRAEL na kuiombea lazima MUNGU akupe baraka tu!
Mwanzo 12:1-2 Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa na kukubariki na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka nami nitawabariki wakubarikio, naye akalaaniye nami nitamlaani,
 hizi ni baraka MUNGU alimpa Ibrahim ( Babu yake na Yakobo) kwanini tunazipokea kama ni Baraka za ISRAEL? Ni kwa sababu Tumefungwa na agano la Ibrahim Wagalatia 3:29 Na kama ninyi ni wa kristo basi mmekuwa uzao wa Ibrahim na warithi sawasawa na Ahadi. Nchi ya Israel ni nchi ya Ahadi pia kwetu sisi.

Hivyo basi unatakiwa uwe ni mtu wa kuibariki ISRAEL siku zote kwa sababu Tumefungwa na hili agano la Ibrahim
Kabila 12 zilizotengeneza Taifa la ISRAEL ( Leo Tutaangalia 2)
Rubeni: huyu alikuwa ni mzaliwa wa kwanza Yakobo.
Rubeni alilaaniwa na Baba yake Kosa lake ni Alitembea na mke au suria wa  Baba yake aitwaye Bilha. Mwanzo 35:22 Ikawa Yakobo alipokuwa akikaa nchi ile Rubeni akaenda akalala na Bilha suria wa Babaye Yakobo akasikia Habari hii
mwanzo 49:3 wakati Yakobo anatoa Baraka kwa watoto wake alimwambia Rubeni "Rubeni u mzaliwa wangu wa kwanza nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu
 Umeruka mpaka kama maji basi nakuondelea ukuu kwa sababu ulikipanda kitanda cha Baba yako.Hapa Kabila la Rubeni linahesabika kama ni kabila lililopotea na kugawanyika kwa sababu alilalaaniwa na Baba yake. Kwa sasa uzao wa Rubeni umepotea haupo ISRAEL
Kabila la Simeon na Lawi
Simeon alikuwa na mtoto wa Yakobo alifuatana na mdogo wake Lawi!  Hawa Nao waligawanywa ISRAEL.

Uzao wao ulipotea na Kosa alilofanya Simon na Lawi ni
Mwanzo 34: kuna habari za Dina Dada yao na akina Simon na lawi alibakwa na Kijana wa kijiji cha jirani aitwaye Shekemu akamtoa usichana wake, baadaye Baba yake Shekemu Mzee Hamori akaenda kuomba
Msamaha kwa Yakobo wazazi wa Dina akaahidi kulipa mahari na gharama zote na Shekemu yupo tayari kumuoa Dina, lakini Simon na Lawi walikasirika kitendo alichofanyiwa Dada yao Dina wakavamia kijiji cha akina Shekemu wakawauawa Wanaume wote na Shekemu akauliwa na Baba yake.

Wakamchukua Dada yao
Sasa katika Mwanzo 49: 5 Wakati Yakobo anatoa Baraka kwa Simon na Lawi walilaaniwa akasema Simon na Lawi Panga zao ni jeuri Nitawagawa katika Yakobo na nitawagawa katika ISRAEL.
Kabila la Simon halipo ISRAEL inasemekana limepotelea Palestina ya kusini
Je Migogoro gani inaikumba Taifa la ISRAEL
Mgogoro kati ya Israel na Palestina katika kugombea Mji wa Yerusalemu
Mgogoro kati ya ISRAEL na Taifa la Syria katika kugombea Eneo lenye rutuba Golan Heights
Ni maeneo gani yalikuwa katika Taifa la Israel na sasa yamegawanywa?
Kutokana na mgogoro kati ya Israel na Palestina baadhi ya maeneo yamegawanywa na yapo Palestina, mfano Yeriko, Bethelehem na Hebron
Hivyo basi ukiombea ISRAEL usisahau kuombea mipaka yake .
MUNGU awabariki sana wapendwa .

Info:-Email : josephelisa@yahoo.com
Contact: +255 718 66 29 59
Joseph Elisa ( PhD Cand)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni