Scott Highberger aliyekuwa mhalifu na muathirika wa madawa ya kulevya ambaye ambaye kwasasa ni mchungaji ameendelea na harakati ya kutangaza ushuhuda wake kupitia kitabu chake kiitwacho Behind The Wire huku akiwatia moyo wafungwa hao kuwa ndoto za maisha yao zinaweza kutimia hatawakiwa ndani ya gereza.
Mchungaji huyo ambaye kabla hajaokoka aliwahi kukamatwa zaidi ya mara 35 kutokana na mfululizo wa matukio yake mabaya ya kihalifu na uuzaji wa madawa ya kulevya yaliyompa hatia nane zilizopelekea kufungwa mara nane gerezani ambapo baadae alibadilisha maisha yake na kumfuata Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake.
Mara ya kwanza Scott Highberger alikamatwa akiwa na umri wa miaka 12 tu akiwa huko Michigan City, Indiana, alipokuwa akifanya uhalifu na uuzaji wa madawa ya kulevya akiwa katika umri mdogo sana.
“Nilikuwa mtoto mwenye hasira ambaye nilijifunza jinsi ya kutatua matatizo yangu kwa njia ya vurugu na uhalifu,” aliiambia The Christian Post. ” Kwa wakati huo, nilianza kunywa pombe, na tabia hiyo ilianza kunipa athari ya kufanya uhalifu na kutumia madawa ya kulevya.” – alisema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni