Papa Francis amewataka watu wanaoishi katika nchi zilizoendelea kuishi maisha ya kawaida na kupunguza anasa.
Pia amekemea pengo kubwa lililopo duniani baina ya masikini na
matajiri, na kutaka watu watilie maanani katika kuyaendea maisha yao
kuwa Yesu alizaliwa kwenye umasikini, kwenye hori la kulishia ng’ombe.Papa amaeyaongea hayo wakati akiongoza Misa ya Mkesha wa Krismasi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Hii ni Krismasi ya sita kwa Papa Farncis, 82, akiwa kama kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani.
Katika mahubiri yake, Papa amesisitiza kuwa kuzaliwa kwa Kristo kunaashiria mfumo mpya wa maisha “si ya ulafi na kuhodhi bali kutoa na kugawa kwa wengine pia.”
Hebu tujiulize: Je ni kweli nahitaji mali zote hizi na vitu vingine vinavyochangia maisha kuwa magumu? Je naweza kuishi maisha bila kuwa na vitu vya ziada ambavyo si vya msingi na kufanya maisha yangu kuwa mepesi?”
“Kwa waliowengi, maana ya maisha inapatikana katika kumiliki mali na kuwa na ziada ya kutosha. Kiu hii ya ulafi inamulika historia yote ya mwanadamu, hata leo, wachache wanapata mlo wa anasa wakati wengi wanashindwa walau kupata mkate wao wa kila siku wanaohitaji ili kuweza kuishi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni