Baada ya kufanya vizuri kupitia video ya wimbo wake uitwao Afya ya Roho aliouachia mwezi Mei 2018 kwa mara nyingine tena mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Abeid Makarabo ameachia wimbo wake mpya uitwao Nitengeneze uliotayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prudyuza Lameck Mipawa.
“Sisi ni vyombo ambavyo Mungu huvitumia kwa kazi yake, hivyo tunatakiwa kuwa vizuri wakati wote. Ili kuhakikisha kuwa tunatumika katika ufanisi unaofaa ni vizuri kumuomba Mungu atufanyie matengenezo kila kuitwapo leo.
Matengenezo hayo ni pamoja na usafi wa moyo, Wimbo huu unalengo la kukupa nafasi yakujitathmini na kumuomba Mungu akutengeneze katika eneo ambalo kwa namna moja ama nyingine hauko sawasawa na ungependa kuweka sawa mambo yako na Mungu ili akutumie kama chombo chake pendwa.” – Abeid
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri ambao ni imani yetu kuwa utakubariki na kukuinua katika viwango vingine, Barikiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni