Breaking

Jumapili, 20 Januari 2019

James Wachenda Aja na Filamu Walimwengu

James Wachenda
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Marekani James Wachenda amefunguka juu ya ujio wa filamu yake mpya inayokwenda kwa Walimwengu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Akiendelea kuongea Wachenda amesema kuwa filamu hiyo ni ya kwanza kuifanya toka aanze huduma ya uimbaji miaka kadhaa iliyopita na anamiini itakuwa ni filamu ya pekee iliyojaa mafunzo kwa watu wote.
“Filamu hii inaitwa WALIMWENGU inazungumzia tabia za watu wa dunia wanavyofanya na Mungu anavyoweza kubadilisha mtu na hii kwakweli ni filamu inayo onya kuwa pasipo kumuhusisha Mungu hasara yake ni kubwa katika maisha ya leo hasa kwa yule aliye mkristo na hata asiye mkristo.” – alisema Wachenda
Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuipata filamu hii, mialiko ya kihuduma wasiliana na James Wachenda kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 (252) 626-9680
Facebook: James Wachenda
Instagram: @jameswachenda
Youtube: James Wachenda

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni