Kutoka jijini Nairobi Kenya kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 tumekusogezea video ya wimbo mpya kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Nardo Turid.
Video hii imeongozwa na TrueD Pictures, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Teddy B.
Hakuna ni wimbo wa sifa unaoliinua na kulitangaza jina la Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa uwezo na nguvu zake sisi tunapokea Baraka, kwa msalaba wake sisi tumekombolewa, amani na furaha yetu imerejeshwa tena, Hakuna kama yeye aliye mkuu anayetawala mbinguni na duniani.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema nahakika kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kila wakati utakapokuwa unaitazama na kusikiliza wimbo huu, Amen
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Nardo Turid kupitia:
Facebook: Nardo Turid
Instagram: @nardoturidofficial
Youtube: Nardo Turid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni