Breaking

Ijumaa, 22 Mei 2020

Somo : Mji Wa Yeriko


Mwalimu : Mtumishi Joseph Elisa (PhD Cand)

Shalom Wapendwa

Mji wa Yeriko ni mji wa kale sana, kwa sasa Eneo la mji  huu ni sehemu ya  Mamlaka ya Palestina.
Baada ya kifo cha Musa, MUNGU alimchagua Joshua kuwa kiongozi wa Wanaisrael ili waweze kuingia kaanani,



Yoshua 1:9 MUNGU alimwambia Joshua, je si mimi niliyekuamuru uwe hodari na moyo wa ushujaa, usiogope, wala usifadhaike kwa kuwa Bwana MUNGU wako yuko pamoja na wewe kila uendako!
Basi MUNGU akamwambia Yoshua Ondoka vuka huu mto wa Yordani wewe na watu wako hawa muende kwenye nchi niwapayo wana ISRAEL
Ilikuwa ni lazima Waisrael wapite kwanza Yeriko!
Yeriko ulikuwa ni ngome na mji wa vita! Ilimlazimu Joshua awe na mikakati jinsi gani ya kuuteka mji wa Yeriko.

Tambua kwanza Yoshua alitanguliza wapepelezi ili kuuchunguza kwanza mji wa Yeriko
Yoshua 2:1-1 Yoshua mwana wa Nuni akatuma watu wawili kutoka shitimu kwa siri ili kupeleleza akawaambia Enendeni mkaitazame nchi hii ya Yeriko, wakaenda Wakafika nyumbani kwa Kahaba mmoja jina lake RAHABU wakalala huko,
Rahabu akawaficha wale Wapelelezi Darini. Akawaficha kwa mabua ya kitani aliyokuwa ameyatandika darini

HISTORIA YA  RAHABU
Rahabu alikuwa ni kahaba, na alikuwa ana nyumba Yeriko, kazi yake ya Ukahaba Rahabu aliitumia kutunza Ndugu zake na jamaa zake na wote aliishi nao Yeriko katika nyumba yake.
Rahabu japokuwa alikuwa ni kahaba lakini alikuwa na imani kubwa sana
Yoshua 2:8 kabla hawajalala wale wapelelezi Rahabu akawaendea juu Darini akawaambia, Mimi najua Kwamba BWANA amewapa nchi hii ya Yeriko na najua ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa Nchi wanayeyuka mbele yenu, maana tumesikia jinsi BWANA alivyokausha bahari ya shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliowatendea wafalme wawili, waliokuwa huko ng'ambo Sihoni na Ogu, mliwaangamiza kabisa
Mstari 12, Basi nawasihi, niapieni kwa BWANA kwa kuwa nimewatendea hii hisani ya kuwaficha, ninyi kwamba mtaitendea ihisani nyumba ya Baba yangu na tena nipeni alama ya uaminifu, kwamba mtawaponya Baba yangu, mama yangu, ndugu zangu wanaume na wanawake na vitu vyote walivyo navyo na kuokoa Roho zao na kufa.

Hii ndio nyumba ya Kahaba Rahabu kabla haijabomolewa Yeriko

Wapelelezi wakamwambia Rahabu uhai wetu badala ya uhai wenu ikiwa hamuitangazi hii shughuli, Wapepelezi wakamwambia Rahabu Funga hii kamba Nyekundu katika Dirisha utakalotuteremshia, nawe ukusanye ndugu zako wote nyumbani kwako, siku ya kuteka mji wa Yeriko tukiona alama hii nyekundu tutaanza kuokoa Nyumba yako kabla ya kuuteka Mji wa Yeriko!
Sadaka ya Imani ilimfanya Rahabu akaokoka yeye na jamaa na Ndugu zake, Rahabu alikuwa na hofu kubwa na kitu cha MUNGU ndani yake lakini Shetani alimshikilia kwenye Ukahaba  ili kufisha kitu cha Kimungu alichokuwa nacho Rahabu.
Kuuteka mji wa Yeriko

Yoshua 6:2 BWANA akamwambia Joshua tazama nimeutia Yeriko katika mkono wako, nanyi mtauzunguka mji huu mara moja, fanya hivi siku sita, na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za kondoo waume na Sunduku la Agano litatangulia mbele na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, siku ya saba kisha makuhani watapiga tarumbeta zao na kisha watapiga kelele kwa sauti kuu na ukuta wa Yeriko utaanguka.
Wakafanya kama BWANA alivyowaamuru na ukuta wa Yeriko ulianguka
Rahabu aokolewa na nyumba yake
Yoshua 6:22 Nae Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na na vitu vyote alivyo navyo, Ndugu jamaa zake na mali zote.
Rahabu alihifadhiwa ISRAEL


Yoshua 6: 25 Yoshua akamhifadhi yule Rahabu kahaba na watu wa nyumba ya Baba yake na vitu vyote alivyokuwa navyo, naye akakaa ISRAEL mpaka leo.
Rahabu alikuja kuolewa na akatengeneza ukoo wa Mfalme Daudi mwimbaji wa zaburi
Dhambi zetu zijapokuwa nyekundu kama Damu, Glory to God! Huwa zinasafishwa zinakuwa nyeupe kama theluji,  Ukisoma  Mathayo 1:5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese, Yese akamzaa mfalme Daudi,
Hapa tunaona Rahabu na ukahaba wake ya kale yalipita akawa kiumbe kipya akaolewa na akatengeneza ukoo wa Daudi! šŸ‘šŸ‡®šŸ‡±
Mji wa Yeriko baada ya kubomolewa na akina Joshua Kipindi wameteka Yeriko

Yoshua aliulaani mji wa Yeriko.Yoshua 6:26
Naye Yoshua akawaapisha kwa kiapo wakati ule akasema alaaniwe mbele za Bwana mtu mtu atakayeinuka na kujenga tena mji huu wa Yeriko, ataweka msingi kwake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake!
Na maeneo gani ya Kiroho yapo Yeriko,?

CHEMCHEM YA ELISHA
2 Wafalme 2:19 watu wa mjini wakamwambia Elisha angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, lakini maji yake hayafai, na Nchi huzaa mapooza, Elisha akasema nileteeni chombo kipya mtie chumvi ndani yake, wakamletea, akatoka akaenda mpaka ile chemchem maji akaitupa ile chumvi humo ndani, akasema Nimeyaponya maji haya hakutatoka tena huko kufa, wala kuzaa mapooza, hivyo yale maji yakopona mpaka leo!
Kisima cha Elisha kipo Eneo la mji wa zamani wa Yeriko na huwa Wagonjwa wanayatumia sana haya maji kwa ajili ya uponyaji.

MLIMA WA MAJARIBU
Mathayo 4: 2- 11 ni sehemu ambayo Yesu alikuwa kwenye maombi ya mfungo siku 40 na  alijaribiwa na Ibilisi, Adui alimwambia ukiwa wewe ndiwe mwana wa MUNGU, Geuza haya mawe kuwa mkate, Yesu akamjibu imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu,
Eneo la mlima wa majaribu ( Mountain of temptations) lipo jirani kabisa na mji wa Yeriko.
Yesu Aingia kwa Zakayo Yeriko
Luka 19:1-10
Mlima wa Majaribu ambapo Yesu alijaribiwa na Ibilisi

Na alipoingia Yeriko alipita katikati yake, Zakayo alikuwa ni mtoza ushuru, naye alikuwa ni tajiri sana, alitafuta kumuona Yesu kwa sababu ya ufupi wa kimo, akatangulia mbio akapanda juu ya mkuyu, apate kumwona Yesu, Yesu alipofika pale akamwambia Zakayo Shuka, upesi kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani kwako, Akafanya haraka akashuka wakaenda kwa Zakayo! Wengi walinung'unika ameingia kwa mwenye dhambi, Yesu akawajibu Mwana wa Adamu alikuja kutafuta kilichopotea! Zakayo akasema Ee BWANA nusu ya mali yangu nitawapa  maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila nitamrudishia mara nne ! Yesu akasema Zakayo leo Wokovu umeingia Nyumbani kwako
Huu mti wa Zakayo Upo Maeneo ya Yeriko mpaka leo
Mkuyu wa Zakayo uliopo Yeriko
KIPOFU BARTIMAYO MWANA WA TIMAYO
Marko 10:46 -51
Bartimayo Kipofu aliyekuwa akiketi kando ya njia 

Wakafika Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, Bartimayo yule kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia, aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, akapaza sauti akasema Yesu mwana wa Daudi Unirehemu, Yesu akaagiza Bartimayo aitwe, Yesu akamwambia unataka nikufanyie nini? Bartimayo akajibu nataka kuona, Yesu akamwambia Enenda zako imani yako imekuponya! Mara Bartimayo akaona !
MUNGU awabariki sana watumishi!

Info:-Email : josephelisa@yahoo.com
Contact: +255 718 66 29 59
Joseph Elisa ( PhD Cand)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni