Breaking

Ijumaa, 25 Januari 2019

Video | Audio: Barakito Rodrigue – Ubatili

Kutoka nchini Marekani kwa mara ya kwanza leo tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Barakito Rodrigue na hii ni video ya wimbo wake mpya uitwao Ubatili.

Video hii imeongozwa na B Kito Music, Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Joachim Music chini ya mikono ya prodyuza Joachim.
“Katika wimbo huu nazungumzia kuhusu namna gani wanadamu wanatamani mambo ya kidunia. Kwasababu hiyo, Wivu unaingia ndani ya watu na chuki vile vile, Wimbo huu unawaambia na kuwakumbusha watu kwamba wawe ni watu kushukuru kwa yale waliyonayo kwasababu mambo yote hapa chini ya jua ni ubatili mtupu. Pesa, Mali, haya yote yata pita, Jambo jema ni kutafuta kwanza ufalme wa Mungu, na mengine yote tutazidishiwa.” – alisema Barakito
Hii ni moja kati ya nyimbo na video ambazo utazifurahia kutazama na kusikiliza kwa mwaka huu 2019 kwa ujumbe mzuri uliobebwa katika kazi hii, Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Barakito Rodrigue kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 (319) 594-3951
Facebook: Barakito Rodrigue
Instagram: @barakito_official

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni