Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza kabisa katika mwaka 2019 tunaisogeza kwako video mpya inayokwenda kwa jina la Sio Mbali kutoka kwaya ya vijana inayofahamika kwa jina la Kiu Tucas Choir.
Video hii imeongozwa na director Crix Kutoka studio za Maxum Vision zilizopo jijini Dar es salaam.
Sio Mbali ni wimbo wa uamsho unaowakumbusha wanadamu juu ya kuacha maisha ya dhambi na kuuendea wokofu ili kuishi Kitakatifu maana sio mbali dunia itafika mwisho na Bwana atakuja kuchukua wale wote walioshinda dhambi na wale wale wasio wake watalia na kusaga meno maana moto wa milele utakuwa juu yao, Je ulishawahi kujiuliza Bwana akija wewe utakuwa upande gani?
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika kuwa itakubariki kila wakati kwa ujumbe mzito utakaoweka jambo jipya ndani yako, Amen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na uongozi wa kwaya kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 692 021
Facebook: Kiu Tukasa Choir
Instagram: @kiutukasa_choir
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni