Bwana Yesu asifiwe
Ninakukaribisha Tena siku nyingine tuweze kujifunza somo zuri lenye kichwa cha habari kinachosema Furaha ya Bwana.
(Warumi 15:13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.)maandiko yanaonyesha kuwa furaha ya Bwana inakuja pale unapochukua hatua ya kumuamini Mungu na kumtumainia.Kumumini Mungu ni kuwa na hakika kuwa Mungu atajibu mahitaji yako hata kama unapitia mzingira magumu katika maisha yako.Kumtumaini Mungu ni pale tegemeo lako lote linakuwa kwa Mungu peke yake na wala si kwa mwanadamu.Ukiwa na Tumaini pamoja na Imani, furaha ya Mungu inaingia ndani ya moyo wako.
(Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini)maandiko yanatuagiza na kutoa msisitizo kuwa tufurahi siku zote katika Bwana.Mungu anataka tufurahi siku zote hata kama tunapitia katika mateso,katika maumivu ,katika kuachwa na katika changamoto yoyote ile.(Yakobo 1:2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali) Neno hili linatuambia kuwa tuwe na furaha hata kipindi tunapokuwa tunapitia katika majaribu mbalimbali kwani majaribu ni sehemu ya maandalizi ya kuinuliwa kwetu pale tunapoyashinda.Hakuna jambo lolote lisilokuwa na mwisho kwa hiyo hata hayo majaribu unayopitia yana mwisho wake.Kila jambo chini ya jua lina majira na wakati wake, lina mwanzo na pia lina mwisho.
(Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu)kwa hiyo jambo lolote lile gumu unalokutana nalo katika maisha, iwe maumivu,mateso au lolote lile lisikufanye ukose raha,lisikufanye ulie,lisikufanye uwe na mawazo bali muachie Mungu halafu wewe songa mbele.Jukumu lako ni kumkabidhi Mungu kila unalopitia,umshukuru Mungu lakini pia uombe.
(Nehemia 8:10 Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.)maandiko yanasema kuwa Furaha ya Bwana ni nguvu yetu, kwa hiyo ipo Nguvu ya Mungu pale unapokuwa ukiishi maisha ya furaha.Furaha ya Mungu inakupa nguvu ya kusonga mbele,lakini unapoikosa hiyo furaha utabaki hapo hapo ulipo.( Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu)ufalme wa Mungu unaingia ndani yako pale furaha ya Bwana inapotawala katika maisha yako, na ufalme huu unapoingia unakupa kumiliki na kutawala.kwa hiyo ukikosa amani na furaha maishani mwako hutoweza kumiliki.
Ninakushauri siku ya leo amua kuishi maisha yenye furaha na amani hata kama unapitia mazingira magumu.Mkabidhi Mungu maisha yako na kila unachopitia,umshukuru yeye lakini pia uombe.
Mungu akubariki sana.
Kwa ushauri ,pamoja na maombezi unaweza kuwasiliana nami kupitia
Apostle Daniel
Whatsapp: 0756277095
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni