Breaking

Jumapili, 24 Mei 2020

Somo : Bahari ya Chumvi Dead Sea


Bahari ya Chumvi Dead Sea ISRAEL

Mwalimu Joseph Elisa (PhD Cand)


Bahari ya chumvi ni Eneo mojawapo lilopo nchini ISRAEL! Watu wengi hutalii eneo hili pia kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya Ngozi, na Vidonda! Bahari ya chumvi Dead sea maji yake ni chumvi pamoja na matope   yake, na watu hutumia matope ya Dead sea kujipaka kama dawa ya magonjwa ya ngozi, scrubbing n.k


Dead sea ni Eneo la Uchumi wa Viwanda kwa Israel
Eneo hili la Dead sea kuna Viwanda vya vipodozi, mbolea, madawa ya binadamu, hivi viwanda vinafumia malighafi ya madini mbalimbali kama chumvi, phosphates yanayopatikana hapo bahari ya  Dead sea
Viwanda vya mbolea vilivyopo Eneo la Bahari ya Dead sea

Kibibilia pia Eneo hili la Bahari ya chumvi lina historia pia ya akina lutu na Sodoma na Gomora
Mwanzo 19:15-22 hapa pana habari za malaika alienda kumwambia Lutu na mke wake na binti zake waliobakia watoke katika nchi ya Sodoma na Gomora Uovu umezidi! Wahamie nchi nyingine ya Soari! Maana Bwana anataka kuharibu miji ya Sodoma na Gomora kutokana na uchafu uovu uliokuwepo! Na MUNGU aliwapa sharti wakiwa wanaondoka wasitazame nyuma!

Matope ya Dead sea ni Dawa ya magonjwa ya Ngozi

Mstari 23, Jua likiwa limechomoza juu ya Nchi Lutu aliingia Soari, Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto kutoka mbinguni akaangusha miji yote na bonde lote, na wote waliokaa katika mji ule, Lakini mke wake Lutu alitazama nyuma akawa nguzo ya jiwe la Chumvi
Uzao wa lutu ulikuwa unaishi eneo la Jordan valley and Dead sea
Mke wa lutu baada ya kugeuka nyuma akawa jiwe la chumvi
MUNGU awabariki sana
Info:-Email : josephelisa@yahoo.com
Contact: +255 718 66 29 59
Joseph Elisa ( PhD Cand)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni