Kutoka jijini Mwanza kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 leo tumekusogezea wimbo mpya uitwao Naanzia Hapa kutoka kwa David Cosmas akiwa ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo za Injili Tanzania.
“Naanzia Hapa ni wimbo uliobeba ujumbe wa matumaini kwa mtu aliyekata tamaa kwa moyo uliovunjika kutokana na mapito mbalimbali, Haijalishi ni kwa muda gani umekuwa unahangaika kwa hayo unayopitia kumbuka Mungu yupo nawe hajakutupa wala kukuacha mpendwa, Piga magoti kwa ujasiri muombe naye atakusikia na kukujibu sawa na haja ya moyo wako..” – alisema David Cosmas
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu ambao kwa hakika utakubariki na kukuinua kila wakati, Amen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na David Cosmas kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 766 709 443
Facebook: David Cosmas
Instagram: @official_davidcosmas
Youtube: DAVID COSMAS
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni