Breaking

Ijumaa, 11 Januari 2019

Watumiaji wa Simu Janja Waonywa na Mpinga Kristo

Tabia ya watu kutegemea sana simu janja (smart phone) pamoja na teknolojia ya kisasa kunaweza pelekea kuja kwa Mpinga Kristo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Orthodox la Urusi Askofu Kirill ameonya.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Urusi wamejibu ujumbe huo kwa ucheshi na kushuku huku baadhi wakilishutumu kanisa hilo kuwa “linautumikia utawala wa Rais Vladimir Putin.”
Akiwa anaongea na televisheni ya Taifa ya Urusi, Askofu Mkuu Kirill amesema watumiaji wa simu janja wanatakiwa kuwa makini wakiwa wanatumia programu mbali mbali za mtandao kwasababu zimewasilisha “fursa ya kudhibiti binadamu ulimwenguni”.
“Mpinga kristo ni mtu ambaye atakuwa ndio kichwa cha tovuti ulimwenguni akidhibiti binadamu,” amesema.
“Kila mara unapo tumia simu yako janja, bila kujali una penda au hupendi, umewasha progamu ya kuonyesha mahali ulipo au la, kuna mtu anaweza kugundua mahali ulipo, vitu unavyo penda na vitu unavyo viogopa,” Askofu Mkuu Kirill ameiambia Rossiya 1.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni