Breaking

Jumanne, 15 Januari 2019

Video | Sephania Mwahalende – Nikurudishie Nini

Kutoka kwenye albamu yake ya kwanza leo tunaitambulisha video ya wimbo uitwao Nikurudishie Nini kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Sephania Mwahalende.
Nikurudishie Nini ni wimbo unaobeba jina la albamu yake ya kwanza ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo sita katika mfumo wa video DVD ambayo kwasasa inapatikana sokoni.
Huu ni wimbo wa sifa na shukrani kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alifuta dhambi zetu kupitia mateso na msalaba wake, Na sasa tunamtukuza yeye kwa maana wema na fadhili zake ni za milele.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki na kukuinua kila siku, Amen.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni