Baada ya kimya kidogo rapa mkongwe katika huduma ya muziki wa Injili nchini Tanzania maarufu kama Rungu la Yesu ameachia video yake mpya ya wimbo unaokwenda kwa jina la Utakatifu.
Video hii imeongozwa na director Fecha, Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Blessed Music Industry (B. M. I.) chini ya mikono ya prodyuza Eribless akishirikiana na prodyuza Amyz.
“Nineema ya pekee unapoitazama video hii ya Utakatifu kwa mara ya kwanza na kuendelea, usisahau kudondosha maoni yako hapo chini, Asante director Fecha kuhakikisha video ya ngoma hii inamalizika ipasavyo, share kwa wengine waone video hii.” – Rungu la Yesu
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki, Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni