Kutoka mjini Moshi Kilimanjaro kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji mpya katika huduma ya muziki wa Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Mercy Kawogo na huu ni wimbo wake mpya
unaokwenda kwa jina la Mungu Wetu hapa akiwa sambamba na mwanadada anayefahamika kwa jina la Sofia.
Video hii imeongozwa na director Wilsoni Maziku, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono producer Frank Kazili.
“Mungu Wetu ni wimbo wa Sifa uliobeba ujumbe wa kumsifu na kumtukuza Mungu kwa maana hakuna kama yeye anayestahili kusifiwa duniani na mbinguni anatawala yeye Bwana.” – alisema Mercy
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na ni hakika kuwa utabarikiwa, Amen.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Mercy Kawogo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 716 169 357
Facebook: Mercy Kawogo
Instagram: @mercykawogo
Simu/WhatsApp: +255 716 169 357
Facebook: Mercy Kawogo
Instagram: @mercykawogo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni