Breaking

Ijumaa, 18 Januari 2019

Video | Hype Burton – Afadhali

Baada ya wiki chache zilizopita kuachia wimbo uitwao Basi, Kwa mara nyingine tena tunaitambulisha kwako video ya wimbo mpya uitwao Afadhali kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Hype Burton.
Video hii imeongozwa na Frank Temba Films na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Kimamba.
Afadhali ni wimbo unaomkumbusha mtu au kijana aliyepotea kwenye njia ya dhambi na kufanya mambo ambayo hayampendezi Mungu na baadae anagundua kuwa anahitaji kurudi kwa Mungu Baba kwakuwa ameona njia anayoiendea si sahihi katika maisha yake. Na kupitia wimbo huu anakiri kukosea na sasa ameamua kutubu ili azaliwe upya na kuitakasa roho yake.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema iliyobeba ujumbe utakaokwenda kuweka jambo jipya ndani yako na kubadilisha maisha yako, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Hype Burton kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 686 345 452
Facebook: Hype Burton
Instagram: @hypeburtontzz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni