Sylvia Alexander ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam ambaye hivi karibuni amefunguka juu ya ujio wake mpya wa video inayokwenda kwa jina la Nipe Ujasiri.
Sylvia amesema kuwa huu ni ujio wake kwanza kwa mwaka 2019 ikiwa ni moja kati ya kazi zake nzuri anazotarajia kuziachia mwaka huu akiamini zitakwenda kuitangaza Injili na kubadilisha maisha ya watu wengi hasa wale ambao hawajampokea Kristo sawa sawa.
“Nipe Ujasiri ni wimbo uliobeba ujumbe wa kumtia moyo mtu ambaye moyo wake umevunjika kutokana na mapito mbalimbali ya kimaisha, Unajua ndugu yangu katika dunia ya leo kuna vita nyingi sana kama mtu kukatishwa tamaa, kuvunjika moyo, maadui kuwa wengi, misukosuko ya maisha hali inayosababisha mtu kushindwa kuendelea na kudhani kuwa Mungu kamuacha kumbe sivyo, Ndio maana nikaimba wimbo huu nikimwambia Mungu Nipe Ujasiri niweze kuyashinda mapito yangu yote na moyo Wangu aufinyange vile apendavyo.” – alimaliza Sylvia
Kupitia blog yako pendwa endelea kukaa karibu nasi ili uweze kuipokea video hii mpya kutoka kwa mtumishi wa Mungu Sylivia Alexander na hakika utabarikiwa zaidi kuliko unavyodhani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni