Breaking

Ijumaa, 18 Januari 2019

Rose Chipe Atoa Neno la Shukrani

Rose Chipe Atoa Neno la Shukrani
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Arusha Rose Chipe amefunguka kwa kutoa neno lake la shukrani kwa watu wote waliomsapoti na kuipa nguvu huduma yake hasa tangu alipoachia video ya wimbo wake uitwao Hakuna Kama Yesu wiki chache zilizopita.

Akiongea na mwandishi wetu Rose alisema kuwa anawashukuru watu wote waliomsapoti na wanaoendelea kumsapoti katika huduma yake na kwa kiasi kikubwa ameanza kupiga hatua mpya tangu alipoachia video ya wimbo wake Hakuna Kama Yesu.
“Kwanza kabisa Namshukuru Mungu aliyeniwezesha kuitenda kazi yake, Napenda kuwashukuru sana wapenzi na wafuatiliaji wote wa nyimbo za injili kwa kuipokea kazi yangu ya video Hakuna Kama Yesu. Naamini umebarikiwa na video hiyo na Mungu azidi kukubariki kupitia ujumbe huo, Nawashukuru Sana wote wanaoniombea na kuisapoti kazi yangu media, radio na blog zingine zote asanteni sana.” – alisema
“Napenda kuwaomba wapenzi wa nyimbo za injili wakae tayari kuipokea albamu yangu mpya inayoitwa Nimekutana na Yesu ambayo kwasasa iko kwenye maandalizi na muda si mrefu nitaiachia ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane ambayo ndani yake nimewashirikisha waimbaji mbalimbali katika kumtangaza Yesu Kristo kwa ari na nguvu zaidi.” – alimaliza
Kama bado hujawahi kuitazama video ya wimbo Hakuna Kama Yesu, Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kuitazama hapa na usisahau kuweka maoni yako na ku-subscribe katika channel yake, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Rose Chipe kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 621 077 670
Facebook: Rose Chipe
Instagram: @rose_chipe
Youtube: Rose Chipe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni