Breaking

Ijumaa, 18 Januari 2019

Audio | Joshua Mkupi – Mkuu Sana

Kutoka mjini Morogoro kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 leo tumekusogezea wimbo mpya uitwao Mkuu Sana kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Joshua Mkupi.
Huu ni wimbo wa sifa unaolisifu jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwa matendo yake makuu na wimbo huu ni sehemu ya shukrani zetu kwake kwa utukufu wa jina lake.
“MUNGU NI MKUU SANA, HAKUNA KAMA YEYE. NAMSIFU KWA UKUU WAKE MAANA HAKUNA TENA KAMA YEYE. Zaburi 150:1-6” – alisema Joshua
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu wa sifa na hakika utabarikiwa kwa kulisifu jina la Bwana, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Joshua Mkupi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 763 446 177
Facebook: Josh J Mkupi
Instagram: @joshmkupi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni