Breaking

Jumapili, 13 Januari 2019

Video | Dare David – Who Is Like Our God Feat. RNA Messengers

Mwimbaji maarufu kutoka Nchini Nigeria Dare David hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao  Who Is Like Our God akiwa amewashirikisha kundi la waimbaji linalofahamika kwa jina la RNA Messengers. Huu ukiwa ni moja ya wimbo unaopatikana kwenye albamu yake iitwayo “Let Your Glory Fall” aliyoiachia mwaka 2017.
Katika maneno ya Dare mwenyewe alisema, “Kwa kuangalia tu jinsi Mungu alivyokuwa mwema kwangu na familia yangu, siwezi kushaa ukuu wake, Kwa kipindi cha mwaka mzima Mungu amenipa usalama wakati wa safari zangu. Hata wakati mwingine, nilifikiri mwisho wangu umefika, Mungu alijitokeza mwenyewe na akaniokoa mara nyingi. Kwa hiyo, ninamshukuru Mungu kwa fadhili zake za upendo na kutoka moyoni mwangu kwa ulimwengu, naamini kwamba video hii italeta ushuhuda zaidi kwa kila mtu anayeitazama”
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki kweli kweli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni