Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara ya kwanza tunamtambulisha kwako mwimbaji wa nyimbo za Injili mwenye talanta ya pekee ya uimbaji anayefahamika kwa jina la Atu Mwailunga na hii ni video yake mpya inayokwenda kwa jina la Thank You, Hii ikiwa ni moja kati ya nyimbo itakayopatikana kwenye albamu yake tarajiwa inayokwenda kwa jina la UNANIJUA.
Video hii imeongozwa na director Sylvester, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Tripod Music chini ya mikono ya prodyuza Mordens Music.
“Thank You (Asante) ni wimbo uliojaa shukrani mbele za Mungu kwa yale yote ametenda na anayoendelea kututendea kila siku, kila wakati na kila saa, Hata hapa tulipo leo ni kwasababu ya Neema yake kuu katika maisha yetu, Ni yeye pekee anayestahili sifa na shukrani kwa maana matendo yake ni makuu sana.” – Atu Mwailunga
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema itakayokujaza Roho Mtakatifu kila wakati utakapokuwa unaisikiliza na kutazama, Barikiwa!
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Atu Mwailunga kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 788 146 036
Simu/WhatsApp: +255 788 146 036
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni