Breaking

Alhamisi, 3 Januari 2019

Kuna Nguvu katika kunyamaza kutokana na mambo yanayojiinua kwako



36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe.
37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.
38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. MATHAYO.26:36-38

Sio kila jambo linalojiinua mbele yako unapaswa kumwambia kila mtu mapito yako, mengine ni kunyamaza na kunyamaza kwako kutokumwambia kila mtu unayemwona mbele mapito yako kunamfanya Mungu akufunulie hekima ya kukuongoza na kumwona mtu atakayebeba mzigo wako katika maombi, sio kila mtu atakayesikia mapito yako atakuwa na mzigo kubeba mzigo wako na kwenda nao mbele za Mungu hapana!!
Yesu anatufundisha jambo hili kupita hutumishi wake; Ebu check!
Alikuwa na mitume 12 akawakusanya pale katika mlima wa Gethsemane wote 12 alichokifanya katika kundi lote hilo akachagua mitume watatu(3) tu mtume Petro, Yohana na Yakobo akaongozana katika sehemu ya maombezi. Baada ya kuwapiga kisogo wale mitume 9 aliowaacha wameketi pale mlimani, akanza kutoa hisia zake kwa hawa mitume watatu(3) angalia maneno haya;
“Akaanza kuhuzunika na kusononeka.
38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.” Kwa sababu ya kunyamaza kwenye pito lake ndani yake iliinuliwa hekima ambayo ilipata kumwongoza kupata na watu wa kuweza kubeba pito lake katika maombi.
Nataka nikwambie mpendwa hilo pito ulilo nalo mlango haujafunguliwa kwa sababu kila mtu umemfanya bango la pito lako, si kila uliyemwambia amekuwa na mzigo wa kulisogeza mbele za Mungu wengine ndiyo umewapa namna ya kupata kick kujulikana mtaani kwa kusambaza habari zako pengine usingemwambia angekuwa busy na mambo yake mengine.
Wengine ulipomwambia pito lako mmeishia kuumizana na urafiki wenu umevunjika kwa jinsi alivyosema udhaifu wako kwa watu na kukudharau, sishangai jambo hilo badala yake najifunza kunyamaza kupitia Yesu Kristo alijua kwamba hayo yaliyotokana na kusema sema kwako kwa kumwambia kila mtu yangempata aliwachagua mitume wake watatu(3) tu alijua sio wote watafurahia jambo lililojiinua kwake, na sio wote watauzunika na kumtia moyo kwa namna ya kuzidi kumwombea mbele za Mungu, alijua mitume wake vizuri viwango vyao vya imani vilitofautiana kama ilivyo makanisani mwetu na jamii iliyotuzunguka kwa ujumla.
Kuna jambo ambalo mtoto anajua kwamba hili siwezi kumwambia baba hawezi kulibeba kwa mzigo na kunisaidia badala yake anakimbia kumwambia mama yake akijua kwa mama anaweza kupata msaada wowote hata kutoka kwa baba lakini kupitia kwa mama, anajua kuna namna mama anaweza akaongea na baba yake na baba akapata kumsaidia kuliko kama angeenda moja kwa moja kwa baba yake msaada usingetoka.
Piga picha kama taarifa ya Yesu kuugua moyoni kiasi cha kutaka kufa kama ingemfikia TOMASO maskioni mwake ingekuwaje? Yesu alikuwa anatufundisha kutumia hekima juu ya mapito tunayopitia kwa kunyamaza sio kumwambia kila mmoja jambo lako, wengine watavunjika moyo kwa kushindwa kumwamini Mungu wako, ndicho Yesu alichokiona ndani ya baadhi ya wanafunzi wake, tunamwona Tomaso kiwango chake cha imani kilikuwa kidogo na sio yeye tu wapo wengi hata wakina Yuda wangeshindwa kumwamini tena kuwa ni Mwana wa Mungu, wangemwona ni mtapeli tu Mungu gani anakuacha wewe, sisi tumekukimbilia wewe ili tuokolewe kumbe na wewe ni mdhaifu?
Kama wewe ni mchungaji au una kundi nyuma linalokufuata au una watu unawaongoza katika nafasi yoyote uliopo chunga sana mapito yako waumini au wale unaowaongozo wasije wakayasikia watashindwa kukuamini, utawavunja moyo juu ya huduma yako watakuona ni mtapeli tu. Kumbe sio mtapeli bali ni mapito katika safari ya mbinguni kwa kuwa wameshindwa kulibeba pito lako ndiyo maana wamekuona hufai.
Lakini kama ungenyamaza Mungu angekuinulia watu wa kuweza kubeba pito lako na kuweza kwenda nao kukesha wakiliombea kama Yesu alivyopata wa kuombea pito lake, check! 38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. Hawa mitume wakakesha nae, yaani wakadumu katika kuliombea pito lake, kuwa na partiners prayer ni kuzuri sana.
Endapo angeongea mbele ya wale mitume juu ya pito hilo si ajabu wengi wao wangesambaa na kuondoka mjini na kuita waandishi wa habari kutangaza kwamba “Bwana yule mtu tuliyekuwa naye, tuliyekuwa tukizunguka naye huku na huko ni mwuuni mwuuni tu mtapeli hakuna kitu sio Mwana wa Mungu!!!!!!!!” Kwa hiyo tatizo lake lisingekuwa limepata msaada angeishia kujenga chuki na visasi kwa hao aliowambia mapito yake.
Check! Wale wote katika jamii iliyotuzunguka ambao wamejengeana chuki na visasi ni baada ya kusikia mwenzake kavujisha mambo yake, jifunze kunyamaza mwana wa Mungu katika mambo unayopitia sema na Mungu tu angalia hekima ya mtu ambaye ataweza kubeba pito lako, Yesu alitufundisha ni jambo jema kuwashirikisha wenzetu mapito yetu maana hata yeye aliwambia wale mitume wake watatu; mtume Petro, Yohana na Yakobo kwamba wakeshe pamoja maana yake waliatamie pito lake aliwaacha wale wengine tisa(9).

KUNYAMAZA NI ISHARA YA NINI?
1.Kunyamaza ni ishara ya UFAHAMU.
12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.MITHALI.11:12
Mpendwa kunyamaza kwako kutakufanya Mungu akuone wa thamani kuliko kujionyesha kwa wanadamu unajua kuongea alafu ukakosa thawabu mbele za Mungu na mwenye ufahamu katika neno lake.
2.Kunyamaza ni ishara ya UTII.
Kutii ni kuonyesha kumpenda Mungu ndipo na Mungu anapokuinua kutoka kwenye pito unalolipitia, lakini unapoinua kinywa chako kusema kwa kila mtu mapito yako utakosa msaada kwa Mungu.Yesu aliponyamaza na kuwa mtii kwa Mungu na Mungu akamkirimia jina lipitalo majina yote, maana yake akampa mamlaka yote mbinguni na duniani.
8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. FILIPI.2:8-11
3.Kunyamaza ni ishara ya UNYENYEKEVU.
Unyenyekevu ni kuonyesha kuwa unahitaji msaada toka kwa Mungu kwa njia yako wewe huwezi juu ya pito ulilo nalo;
6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. 1 PETRO.5:6-7

Mpendwa mpe nafasi Mungu ya kukutetea katika wingi wa maneno yako kwa watu hakuna mlango wa Mungu kukutetea, badala yake unajinajisi tu na msaada hutauona kwenye wingi wa maneno yako, nyamaza Mungu mwenyewe atakukweza kwa wakati wake. Kusema sema ovyo kwa kila mtu ni ishara ya kutokumpa Mungu nafasi ya Yeye kukupigania ni ishara ya kujiinua kabla ya wakati wako.
Tafakari hilo somo letu la leo kwa dhumuni la kutaka kumzalia Mungu matunda, na pale ulipokuwa umekosea kwa kusambaza habari zako kwa kila mtu omba toba kwa sababu ya jambo hilo. Tazama kusema sema kumekufanya ukosane na ndugu na jamaa wale ambao ulidhania wamekusema vibaya na kuwa na uhasama nao, omba toba Mungu atakusamehe.Nikushukuru mwana wa Mungu uliyefuatana na mimi tangu mwanzo wa somo letu UBARIKIWE SANA.
BY
MWL.EDWIN KASHALABA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni