Mafanikio makubwa ya filamu za Kikristo katika miaka ya hivi karibuni umesababisha kuwa na ushinikizo mkubwa wa utengezaji wa filamu hizo huko Hollywood.
Mwaka wa 2018, filamu ya “I Can Only Imagine” ilipata mapato ya kiasi cha dola za kimarekani $ 17.1 milioni ndani ya wiki moja tangu kuzinduliwa kwake. Na filamu ya “Paul, Apostle of Christ” ilikuwa kati ya filamu 10 bora duniani wiki moja tangu kuzinduliwa kwake.
2019 unatarajiwa kuwa ni mwaka mwingine mkubwa kwa filamu za Kikristo zinazotarajiwa kuachiwa, Na hii hapa ni orodha ya filamu tano kubwa za kikristo zinazotajwa kuachiwa mapema mwaka huu.
1. ‘The Least of These’
Kuachiwa: Februari 1, 2019.
Kuachiwa: Februari 1, 2019.
Hii ni filamu ya kwanza ya Kikristo itakayoachiwa mwaka huu ikiwa ni hadithi ya kweli inayomhusu Mmisionari Graham Staines aliyeuawa nchini India mwaka 1999, Ambaye mwanzoni jina lake lilifahamika kama “Staines,”.
2. ‘Heavenly Deposit’
Kuachiwa : Februari 10, 2019
Kuachiwa : Februari 10, 2019
“Heavenly Deposit” ni filamu iliyoongozwa na Rick Irvin na mwandishi wa filamu, Pia akiwa ni mwigizaji wa muda mrefu George Vincent.
3. ‘Run the Race’
Kuachiwa : Februari 22, 2019
Kuachiwa : Februari 22, 2019
“Run the Race” Ni filamu inayolenga kuonyesha uwezekano wa kutokea kwa mabadiliko ndani ya mtu anayetenda mambo yanayomuweka mbali na upendo wa Mungu.
4. ‘XL: The Temptation of Christ’
Kuachiwa : Marchi 6, 2019
Kuachiwa : Marchi 6, 2019
“The Temptation of Christ” Ni filamu inayotoa “mfano halisi” wa majaribu ambayo Kristo alikabiliana na Shetani baada ya kufunga kwa siku 40 Kwa mujibu wa Injili ya Mathayo, Marko na Luka.
“Filamu hii itatumika kama chombo chenye nguvu ya kusaidia wengine kuingia katika imani. Safari ya jangwani inapaswa kuwakilisha kitu cha kujifunza kwa sisi sote na Kufahamu umuhimu Kristo na kukataa kwake dhambi akiwa katika mfungo wa siku 40.
5. ‘The Islands’
Kuachiwa : Marchi 22, 2019
Kuachiwa : Marchi 22, 2019
Ni filamu hiyo yenye hadithi ya kweli inayomhusu Malkia wa Hawaii ambaye aliamua kufuata imani ya Yesu Kristo zaidi ya miaka 200 iliyopita. Uongofu wake ulileta athari ya mabadiliko ya Ukristo kwa visiwa vyote vya Hawaii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni