Breaking

Alhamisi, 3 Januari 2019

Ritha Komba Ajipanga Kuja na Wimbo Wake Mpya



Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Ritha Komba ameweka wazi juu ya ujio wa wimbo wake mpya uitwao Nasimama mapema mwezi huu.
Akiongea na Gospolsharom Ritha amesema kuwa ujio wa wimbo huo utakuwa ni wa kipekee na wa tofauti sana na ilivyozoeleka katika masikio ya watu wengi ambao tayari wameshazisikia kazi zake alizowahi kuachia miaka miwili iliyopita.
“Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kuvuka mwaka mwingine hakika si kwa nguvu zangu bali ni kwa mkono wa Mungu ulioniwezesha leo kuwaletea habari njema juu ya wimbo na video yangu mpya iitwayo Nasimama ikiwa ni wimbo wangu wa kwanza kabisa kuachia kwa mwaka 2019, Hakika wimbo huu utakwenda kumbariki na kumgusa kila mmoja atakayeupokea, Naomba watu wote muendelee kusubiri baraka hizi kubwa, Naamini Mungu atakwenda kufanya jambo jipya kwa ajili ya watu wake, Amen.” – alisema Ritha

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni