Kanisa jipya la Coptic lililojengwa mashariki ya mji mkuu Misri, Cairo limefunguliwa rasmi, Kanisa hilo kuu jipya liliendesha misa yake ya kwanza chini ya ulinzi mkali jumapili ya mkesha wa Krismasi.
- Mhalifu Aamua Kutangaza Ushuhuda Wake na Kuihubiri Injili Gerezani
Ufunguzi wa kanisa hilo jipya lenye uwezo kutosha watu 8,000 limeonekana kumfurahisha sana Rais wa Marekani Donald Trump na kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Nafurahia sana kuwaona marafiki zetu wa Misri wakifungua kanisa kubwa zaidi Mashariki ya Kati. Rais El-Sisi anaongoza taifa hilo kwenye siku za usoni za kuwajumuisha wote!”
Waumini wa madhehebu ya Coptic ni 10% ya raia wote nchini Misri ambako idadi kubwa ya watu ni Wislamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni