Frank Rahaya Albertson au unaweza kumwita Frank Albertson ni mwimbaji wa nyimbo za Injili mwenye asili ya nchi ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye kwasasa anaishi nchini marekani.
Leo tumekusogezea mambo 5 muhimu unayotakiwa kuyafahamu kuhusu mwimbaji huyu:
1. Frank Albertson amezaliwa mnamo tarehe 1 Mei 1992 nchini DRC Congo
2. Frank Albertson amekua katika nchini ya Tanzania na alianza huduma ya uimbaji akiwa katika umri mdogo sana na kuendelea hivyo mpaka alipofanikiwa kuhamia nchini marekani mwaka 2010.
3. Mbali na uimbaji wa nyimbo za Injili Frank Albertson ana kipaji kikubwa pia cha kupiga vyombo kanisani kama vile Gita, Kinanda na Drums mbali na kupiga vyombo pia ni mtunzi mzuri wa nyimbo za Injili.
4. Katika safari yake ya uimbaji hapakuwa na mtu yeyote wa karibu yake aliyetambua kipaji chake mpaka wakati alipoachia wimbo wake wa kwanza uliopokelewa vizuri na kuwashangaza wengi.
5. Ana amini kuwa unapokuwa na kipaji cha Uimbaji basi ni lazima ujitahidi ukitangaze ili Mungu aweze kuonekana kupitia kwa wanaobarikiwa kwa kazi au huduma yako.
“Wakati mwingine ni lazima utangazie mataifa kipaji chako kwa maana unapoogopa na kukifungia ndani Mungu anaweza kumpa mtu mwingine, Bado nina imani kuwa huu ni mwanzo tu mambo mazuri yanakuja kwa ajili ya kuitangaza Injili kwa watu wote, Mungu awabariki sana wote wanaoendelea kuniombea na kunisapoti katika huduma yangu Amen.” – alisema Frank
Kama bado hujapata nafasi ya kutazama video ya wimbo wake uitwao Nisamehe hii Hapa tumekusogezea, Usisahau Ku-comment, Ku-Kulike na Ku-Subscribe ili uendelee kubarikiwa.
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi wa Mungu Frank Albertson kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 (319) 400-4290
Facebook: Frank Esco
Instagram: @_frankesco
Youtube: Frank Albertson
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni