Video hii imeongozwa na director Dee Moolah, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za TopClass Records chini ya mikono ya prodyuza Edgar Mpangile.
“Upo Juu ni wimbo wa sifa unaotukuza na kulisifu jina la Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikuja duniani kumkomboa mwanadamu na dhambi zake, Katika kuadhimisha kuzaliwa kwa mfalme wetu Yesu wimbo huu unatukumbusha kumsifu Mungu na kutambua kuwa yeye ndiye pekee aliye juu ya vitu vyote duniani na mbinguni, #Uko Juu
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni
hakika itakubariki na kukugusa siku zote utakapokuwa unasikiliza na
kutazama, Heri ya Krismasi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni