Breaking

Alhamisi, 27 Desemba 2018

Video | Borne Kingz – Cypher

 
Baada ya kufanya vizuri mwezi May 2018 kupitia video ya wimbo uitwao Fire kwa mara nyingine tena kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop maarufu kama Borne Kingz wameachia video yao mpya inayokwenda kwa jina la Cypher.


Borne kingz ni kundi linalowaunganisha vijana wanne ambao ni Ellyjoh, Lamasias, Elandre pamoja na Quality. Kundi hili liliundwa tangu mwaka 2011 likiwa na vijana watatu kwa nia njema ya kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Maana halisi au kirefu cha BORNE KINGZ ni “Bearing the Mark of the King” ikimaanisha “Wabeba Chapa ya Kifalme”.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa, Ameen.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni