Breaking

Alhamisi, 27 Desemba 2018

Huruma Atoa Ujumbe Mzito kwa Wanawake


Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania Huruma Mbogela kupitia ukurasa wa Instagram alitoa ujumbe mzito kwa wanawake wote ukisisitiza juu ya nguvu ya kujitambu, Upendo na mshikamano.
Ujumbe huo alioutoa siku ya Krismas ukiwataka wanawake wote kujitambua na kutobweteka na mambo ya dunia kwa kuwa shetani huwa anawatumia wanawake kuharibu kusudi la Mungu duniani.
“UJUMBE KWA KILA MWANAMKE


Women are gatekeepers, Namaanisha wanawake ni walinzi. Shetani analijua hilo na ndio maana, moja kati ya maarifa ambayo hatopenda mwanamke ayafahamu ni kuhusu ukweli huu.
Anamsahaulisha mwanamke na usisahau mlinzi akiwa dhaifu, vitu vinavyolindwa vitaibwa tu.
Mengi ya Baraka yameibwa yameharibiwa na adui anayaharibu, kwa kuwa tu waliotakiwa kulinda wameacha wajibu wao na wameanza mengine.

Leo wanawake wako bize na kusengenyana wao kwa wao,kuoneana wivu,wako bize na kuponya maumivu ya kuvuliwa nguo na kuachwa na hao waliodhani watawaoa.
Sikia hii ndugu mwanamke wakati wote mwizi anapotaka kuiba na kuharibu ataanza na walio malangoni. Wewe unadhani, walinzi wakianza kugombana wao kwa wao nini kitatokea??
Wanawake hawapendani wao kwa wao hujawahi kujiuliza why?? Shetani anajua akiwaacha washikamane watakua na nguvu na watamshinda kweli kweli.

My friend usalama wa Familia ndoa kanisa na hata Taifa kwa ujumla unategemea nguvu ya waliokaa malangoni(wanawake), Ndio maana Mungu anawataka wanawake wawe waombaji sana. Ule muda mwanamke unaolipa na kufanya mengine yasiyo ya faida basi ungewekeza kwenye maombi mambo yangebadilika na kukaa mahala pake.
LIPA GHARAMA YA MAOMBI KWA KILA KITU, USIBWETEKE.
Na Mwl. Huruma Mbogela”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni