Video hii imeongozwa na director Mbagwa, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Ritha’s Records chini ya mikono ya prodyuza Kingson na Papaa Denilson.
“Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kuandaa wimbo huu wa NITASHINDA TU ukiwa ni wimbo uliobeba ujumbe wa Roho Mtakatifu kwa watu wote, Ni wimbo Unaomtia mtu moyo aweze kusimama katika neno la Mungu hata kama wanakutana na hali ngumu inayoonekana kama usiku kwao. Mungu anatuwazia mema na ametuhakikishia ushindi, Akiwa upande wetu hatutaogopa wala kutikisika, tuna UJASIRI, Mungu akubariki unapousikiliza kila siku.” – alisema Sayuni Mrita.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki na kukuinua kila wakati utapokuwa unatazama na kusikiliza, Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni