Mwalimu : Joseph Elisa ( PhD Cand.)
Bethlehem inajulikana kama mji wa Daudi, maana ya neno Bethlehem kiebrania ni Beth- house na Lehem- mkate ("house bread" ) nyumba ya mikate. Tafsiri ya bibilia ya kingereza John 6:35-40 Jesus declared himself Iam the Bread of life whoever come to me will never go hunger, Yesu hapa alisema yeye ni mkate wa uzima na yeye aendaye kwake hataona njaa kamwe, hivyo Basi Bethlehem alizaliwa Yesu kristo, Wayahudi wanaamini kwamba mkate wa uzima upo Bethlehem! Kwa sasa mji wa Bethlehem ni sehemu ya mamlaka ya Palestina
Historia gani za kiroho na kibibilia zinapatikana katika mji wa Bethlehem ?
Kuzaliwa kwa Yesu
Hori alipozaliwa Yesu kristo
Konde la wachungaji Bethlehem! Walikuwa wanachunga kondoo usiku wakatokewa na malaika kuelezwa habari za Yesu kuzaliwa
Bethlehem pia inajulikana ni mji wa Daudi, pia Bethlehem ilikuwa ni sehemu ya uzao wa kabila la Yuda " ndio maana sehemu nyingine kwenye maandiko inasema Bethlehem ya Yuda" Eneo hilo alilozaliwa Yesu kwa sasa pana Kanisa lipo "Church of Nativity" ndani ya hilo kanisa kuna hori sehemu aliyozaliwa Bwana wetu Yesu kristo .
Yesu aliitwa Imanueli maana yake mathayo 1:23 MUNGU pamoja nasi
Wachungaji wa Makondeni ( Shepherds)
Bethlehem jirani kabisa na sehemu aliyozaliwa Yesu pana konde walilokaa wachungaji waliokuwa wakichunga kondoo kwa zamu usiku, katika konde hili wachungaji walitokewa na malaika wa Bwana siku ile Yesu anazaliwa usiku
akawaambia Luka 2:10 msiogope kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote, maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa mwokozi ndiye kristo Bwana , wachungaji walikuwa ni watu wa kwanza kupata habari njema za kuzaliwa kwa Yesu, na walienda mbio kumtazama Yesu katika hori hapo hapo Bethlehem
Pia Hili konde ndio Daudi akiwa kijana alikuwa anatumia kuchunga kondoo wa Baba yake Yese Mbethelehemi ! Baada ya Daudi kuchunga kondoo wa Baba yake kwa uaminifu na kuweza kupambana na dubu na simba ilikuwa ni kigezo cha kupata kibali mbele za Bwana na MUNGU alimtuma Nabii Samweli aondoke na pembe ya mafuta aende kwenye nyumba ya Yese ampake Daudi mafuta ya kibali awe mfalme badala ya Sauli
Historia ya Raheli na kaburi la Raheli Bethlehem
Kaburi la Raheli lililopo Efrathi Bethlehem
Yakobo na Raheli walikuwa wanasafiri hata wakafika njia ya Efrathi ndio Bethelehem kwa sasa! Mwanzo 35:16-20, Raheli alishikwa uchungu wa kuzaa na uchungu ulikuwa mzito, wakati anakaribia kumtoa mtoto roho yake ikawa inakaribia kufa, akasema huyu mwana aitwe Benoni maana yake mtoto wa majonzi au maumivu (child of pain or sorrow ) Yakobo akabadilisha jina akamwita mtoto Benjamen maana yake ni (son of right hand) Raheli akakata roho, akazikwa njia ya Efrathi Bethlehem,
hapa tunaona Yakobo aliona nguvu ya jina katika ulimwengu wa Roho akalibadilisha Benjamen asiitwe Benoni uchungu, baadaye tunaona Benjamen alibarikiwa na kutengeneza Taifa la ISRAEL kupitia zile kabila 12 za uzao wa Yakobo
Historia ya Naomi Bethlehem
Kitabu cha Ruthu 1 na 2 kuna mtu aliitwa Elimeleki na mke wake Naomi waliishi Bethlehemu ya Yuda wakabahatika kuwa na watoto wawili Maloni na Kilioni, ikatokea njaa Bethlehem ikabidi Elimeleki na Naomi wahamie Nchi ya Moabu ambayo ni Nchi ya JORDAN kwa sasa, walipokaa Moabu ( Jordan) mumewe Naomi Elimeleki akafariki. Watoto wa Naomi wakakua wakaoa wanawake wa Kimoabi ambao ni Orpa na Ruthu. Orpa alikuwa ni mke wa Kilioni na Ruthu akawa mke wa Maloni, Baadaye wakafariki watoto wa Naomi akabaki na wakweze tu kule Moabu( Jordan)
Naomi alipata majonzi sana hadi aliomba jina lake libadilishwe kutoka Naomi ( kupendeza) aitwe mara ( uchungu)
Baada ya kufiwa na watoto na mume kule Moabu Naomi akawa anataka arudi nyumbani Bethlehem, Naomi akawaambia wakweze Orpa na Ruthu warejee majumbani kwao, wasirudi nae Bethelehem, Orpa alikubali akamuaga mama mkwe wake akarudi kwao, Lakini Ruthu alikataa
Ruthu 1:16 usinisihi nikuache, maana wewe uendako nitakwenda, na ukaapo nitakaa, watu wako watakuwa jamaa zangu, na MUNGU wako atakuwa MUNGU wangu!
Hapo Tunaona Orpa alimkatalia mama mkwe wake, alimpa kisogo! Maana ya jina la Orpa ni Kisogo ( fawn)
Ruthu alirudi na mama mkwe wake Naomi Bethlehemu na wakaanza maisha mapya, Ruthu alifanyika baraka sana kwa Naomi na alimpenda sana mama Mkwe wake na Akimtunza sana! Pia Ruthu alimpenda na kumheshimu MUNGU wa Mama mkwe Naomi, Ruthu alipata tena kibali akaolewa na Boazi pale Bethelehem alikuwa Tajiri na mkulima! Boazi alikuwa ni mtoto wa Rahabu yule aliyekuwa kahaba wa Yeriko, Rahabu alimzaa Boazi baada ya kuolewa na Salmoni, Ruth waliishi maisha ya furaha na Boazi wakamzaa Obedi, obedi ndio alikuja kumzaa Yese, Yese akamzaa mfalme Daudi!
Kiambatanisho cha Majina
Bethlehem - house bread
Orpa maana yake ni fawn /kisogo / back
Imanueli MUNGU pamoja nasi ( Mathayo 1:23)
Naomi ni kupendeza
Mara ni uchungu
Benon ni mtoto wa maumivu/majonzi/child of pain
Benjamen child of right hand
Moabu ( Jordan)
God bless You !
Info:-Email : josephelisa@yahoo.com
Contact: +255 718 66 29 59
Joseph Elisa ( PhD Cand)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni