Breaking

Alhamisi, 21 Mei 2020

Somo :- Mji Wa Jerusalem


Mwalimu : Mtumishi Joseph Elisa (PhD Cand)

Shalom watumishi, natumaini mnaendelea vizuri , leo Tutaangalia Mji wa Jerusalem kiroho na migogoro iliyopo  pale! Karibuni
Utangulizi
Mji wa Jerusalem upo katika Nchi ya ISRAEL, ni mji ambao umegawanyika mara mbili Jerusalem magharibi na Jerusalem mashariki. Jerusalem Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu na Jerusalem mashariki hutazamwa kama Mji mkuu wa Palestina litakapoundwa, Ingawa bado Maeneo yote hayo yametawaliwa na kukaliwa na ISRAEL tangu mwaka 1967 ambapo kulikuwa na vita ya siku sita kati ya Waisrael na Waarabu na ISRAEL alishinda, Mwaka 1973 ilipigwa vita nyingine muungano wa Syria na Misri dhidi ya ISRAEL vita iliitwa  Yom Kippur war"  Israel ilishinda katika vita, mwaka 1980 Taifa la ISRAEL lilitangaza Jerusalem yote ni   mji wake mkuu wa milele. Baadhi ya Nchi duniani hazikubaliani na azimio hilo, hii imepelekea Jerusalem kuwa mgogoro na Balozi nyingi zilizopo ISRAEL ofisi zao zipo maeneo ya Mji wa Tel Aviv. 


Jerusalem ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kujengwa tena. Marekani ilitambua  Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel Dec 2018 na mei 2018 Nchi ya Guetamala ilitambua pia Jerusalem ni mji mkuu wa Israel na mataifa haya yalihamishia Balozi zake Jerusalem .
Bibilia inaizungumziaje Jerusalem ?
Isaya 62:6 Nimeweka walinzi  juu ya kuta zako Ee Yerusalemu hawatanyamaza mchana wala usiku, ninyi wenye kumkumbusha BWANA msiwe na kimya mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu na kuwa sifa kuu Duniani.
Ezekieli 26:2 Yerusalem ni lango la kabila za watu
Mpaka hapo tunaona kwamba Yerusalem
Ni lango la kabila za watu na ni mji wa mfalme mkuu. Yerusalemu pia ni sebule yetu sisi wapendwa wa MUNGU .
Tambua mji wa Jerusalem ni mji unaozozaniwa na Dini kuu tatu!
Mji wa Yerusalem unazozaniwa na dini tatu za UKristo, Uyahudi na Uislamu  ila Dini zote hizi tatu zinamwangazia Abraham ambaye ametajwa kwenye bibilia na kitabu cha korani
Ukristo Yerusalemu
Hapa tunaangalia Agano la Ibrahim kupitia kwa mke halali Sarah na mtoto Isaka  na pia Uzao wa Ibrahim na mjakazi wake Hajiri kwa Heshmail
Mwanzo 21:10 Sarah alimwambia Ibrahim mfukuze mjakazi huyu na mwanawe maana mwana wa mjakazi hatarithi na mwanangu Isaka, Ibrahim aliona hili jambo ni baya lakini MUNGU akamwambia Ibrahim atakalokumbia mke wako Sara fanya kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa ( kumbuka uzao wa Isaka Yakobo ndio umetengeneza kabila 12 za taifa la ISRAEL)
Pia wakati Ibrahim anamfukuza Hajiri na Heshmaili aliwapa Kiriba cha maji na mkate na Hajiri na Heshmail walipotelea Jangwani  Beer sheba na wakiwa Beer sheba maji yaliisha Hajiri akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja asimwone akifa MUNGU akamuonea huruma Hajiri akamfumbua macho akaona kisima cha maji na akamwambia Hajiri nitamfanya Ishamael Taifa kubwa
Wagalatia 4:30 lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana  ndiposa Ndugu zangu sisi si watoto wa mjakazi bali tu watoto wa aliye muungwana
Wagalatia 3:39 Na kama nyie ni wakristo mmekuwa uzao wa Ibrahim na warithi sawa sawa na ahadi
Wagalatia 4:26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi
Hapo Tunaona nini ?
Hapo Tunaona kwamba sisi Wakristo tuliokoka ni wa agano lililo bora kabisa kupitia kwa Ibrahim Sarah na Isaka, Hajiri na Ishmael walifukuzwa
Pili wakati Heshmail anafukuzwa na Mama yake Hajiri hakupewa Urithi kama mtoto wa Ibrahim, alipewa kiriba cha maji na Mkate, mali zote na utajiri wa Ibrahim alipewa mtoto halali wa Ndoa Isaka. Hivyo Heshmail alipewa kama zawadi tu au mkate wa kula kumsaidia njiani katika safari yake mpya! Hakupewa mali kama nyumba, Mashamba, Ngamia, kondoo, zote hizi zilikuwa ni mali ya Isaka mtoto wa Ahadi / mtoto wa Ndoa

Uislamu
Katika mji wa Yerusalem pale pana msikiti wa Al aqsa na waislamu wanaamini Mtume alisafiri kutoka Mecca usiku na aliomba na aliomba pamoja na roho za manabii wengine, Pia wanaamini agano la Ibrahim kwa mjakazi wake Hajiri na Mtoto wake Heshmail wanamwita "Ismail" na wanaamini kwamba  Heshmail ana haki sawa na Isaka kwa sababu alitoka kiunoni mwa Ibrahim na anatakiwa urithi sawa na Isaka
Kiroho iko hivi! Taifa la ISRAEL ni uzao na ufuasi wa agano la Isaka kwa Ibrahim ambapo ni Ukiristo,  Taifa la Palestina ni uzao na ufuasi wa Agano la Ibrahim kwa Hajiri na Ismail
Kisima cha maji alichoonyeshwa Hajiri akamnywesha maji Heshmail ndio kipo Mecca Saudi Arabia  kinaitwa Zam Zam
Tambua Yesu aliuona  mgogoro wa Jerusalem  katika ulimwengu wa Roho ndio maana wakati anaingia Jerusalem alipouona mji aliulilia sana.
Luka 19:42 Ee Yerusalem laiti ungalijua hata wewe katika siku hii yapasayo amani lakini sasa yamefichwa machoni pako kwa kuwa siku zitakapokuja adui zako watakapokujengea boma likuzunguke watakuzingira na kukuhusuru pande zote(Kuhusuru ni kuzunguka kwa vita)
Luka 13:34 Ee Yerusalemu, Yerusalemu uwauwaye manabii na kuwapiga mawe, kwa waliotumwa kwako mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake wala hamkutaka ? ( Hapa tunaona Yesu anawaambia ni mara ngapi nimejaribu kuwaleta pamoja katika meza ya Mazungumzo/usuluhishi  lakini bado mioyo yenu inakua migumu?
Hapa ni wakati Yesu anaingia mji wa Yerusalemu akiwa amepanda mwanapunda!  Siku ya mwisho kabla ya pasaka ( siku ya mitende) Alivyoona mji wa Yerusalemu hali yake ya kiroho ilivyo na vita yake katika ulimwengu wa Roho aliumia sana!
Mji wa Yerusalemu pana hekalu lilojengwa na Mfalme Sulemani na wayahudi wanapaita patakatifu pa patakatifu na pana ukuta wa maombi au maombolezo na wakati Suleiman anajenga alisema haya maombi
1Wafalme 8:41-43
Hata na mgeni naye asiyekuwa mmoja wa watu wako ISRAEL atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako, atakapokuja nakuomba  kuielekea  nyumba hii basi usikie huko mbinguni makao  yako ukatende kwa kadri ya yote utakayokuomba, mgeni huyo ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako na kukucha wewe, kama watu wako Israel nao wajue kuwa nyumba hii niliyojenga imeitwa kwa jina lako ( Hapa tunaona kwanini watu wakienda ukuta wa Maombi wanachomeka vikaratasi vya maombi )

Kumbuka hekalu hilo alilijenga Sulemani na
Hiki kiwanja Baba yake Mfalme Daudi alikinunua kwa Arauna Myebusi! Na Daudi alivyotaka kumjengea MUNGU hekalu alizuiwa na MUNGU akaambiwa mikono yako imejaa Damu uliwauwa Wafilisti,  Sulemani mtoto wako atakuja kunijengea !
Mgogoro mkubwa uliopo Yerusalemu ni mpishano wa kiimani kati yetu Wakiristo na Wenzetu juu ya agano la kiimani kati ya Isaka na Heshmail
MGOGORO WA WEST BANK
Hili Eneo la West bank linatazamana na Yerusalem baada ya vita Israel alijenga nyumba za wahamiaji wa Kiyahudi au walowezi kwenye hili Eneo la Magharibi mwa Yerusalem na wanaishi Wayahudi wengi sana
Na kumekuwa na mgogoro mkubwa kutoka wa Palestina na Mataifa mengine ya kiirabu kwamba hilo Eneo ni la Palestina na ISRAEL anatakiwa ahame hapo!  Pia baadhi ya Nchi za jumuiya ya Ulaya EU na UN wamekuwa wakiisihi ISRAEL iendelee kutawala ( to annex) hili Eneo la Makazi ya Wayahudi kwa sababu wakiondoka litachochea Mgogoro upya au kusababisha tena mapigano kati ya Waisrael na Wapelestina
Je mgogoro huu wa Mji wa Jerusalem na Eneo la West Bank utaishaje kiroho au utatuliwa vipi ? Maandiko yanasemaje ?
Ufunuo 16:16
Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa kiebrania Har - Magedoni
Daniel 2:44  Katika siku ile MUNGU wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake nao utavunja falme hizi vipande vipande za kuziharibu
Hapa tunaona kutakuwa na vita kuu siku ya  mwisho kati ya serikali za wanadamu wale wanaompinga MUNGU,
Na Yesu kristo ataongoza hiyo vita (Kamanda wa Vita) ufunuo 19:11-16 Kisha nikaziona mbingu zimefunguka na Tazama Farasi mweupe na yeye aliyempanda aitwaye mwaminifu na wa kweli naye kwa haki ahukumu na kufanya vita
Hivyo hii vita ya HAR MAGEDONI ndio itamaliza mgogoro wa Jerusalem na Palestina 


MAUAJI YA HALAIKI  YA KIYAHUDI (HOLOCAUST) mwaka 1945
Haya yalikuwa ni mauaji ya Utawala wa kinazi ujerumani na yaliongozwa na Kiongozi wa Kinazi Adolf Hitler
Zaidi ya wayahudi milion 6 waliuwawa kipindi cha vita ya pili ya dunia mwaka 1945
Nchini Israel katika mji wa Jerusalem ipo Makumbusho ya Holocaust yenye picha na kumbukumbu za wayahudi waliouwawa kikatili!
Tar 23 Jan 2020 mwaka huu ilikuwa ni kumbukumbu ya Mauaji ya holocaust miaka 75 na ilifanyika Jerusalem alihudhuria Rais wa wa Ufaransa Emanuel Macron na Mwana Mfalme wa Malkia wa Uingereza Aitwaye Prince Charles
Omba sana Amani iendelee kuwepo kwa Wayahudi na ile amri ya Upendo tuliyoachiwa  na  Bwana wetu Yesu kristo tupendane tuizingatie
Mbarikiwe sana .

Info:-Email : josephelisa@yahoo.com
Contact: +255 718 66 29 59
Joseph Elisa ( PhD Cand)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni