Breaking

Ijumaa, 4 Januari 2019

Yafahamu Matunda 5 yanayoondoa Sumu Mwilini

Kama tunavyojua kwamba miili yetu ina sumu nyingi sana ambazo hazitakiwi kuwepo na sumu hizo mara nyingi zinatokana na vyakula tunavyokula au vinywaji tunavyokunywa bila kujua madhara yake.

Kuna dalili mbalimbali ambazo zitakufanya ugundue kwamba mwili wako una sumu baadhi ya dalili hizo ni kama vile kupata matatizo ya choo yaani choo chako kuwa kigumu, tumbo kujaa gesi, kichwa kuuma kwa muda mrefu huku ukiwa na hasira za mara kwa mara. Lakini haimanishi kwamba usipokuwa na dalili hizo basi mwili wako uko salama.
Habari nzuri ni kuwa kuna baadhi ya matunda tukiyatumia vizuri basi yataondoa sumu katika miili yetu na kutufanya tuwe na afya bora ambayo inatakiwa, baadhi ya matunda hayo ni;
Image result for limao
LIMAO
Limao ni tunda ambalo lina utajiri wa vitamini C ambao husaidia kuondoa chembe haribifu mwilini, chukua limao kamulia kwenye maji kisha kunywa, inasaidia kuondoa sumu mwilini mwako.
PAPAI
Inasaidia kuondoa sumu mwilini na kuupatia nguvu mwili pamoja na kusaidia mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi haraka.
TANGO
Hili tunda ni mojawapo ya matunda yanayosaidia kuondoa sumu mwilini unachotakiwa kufanya ni kukati vipande kadhaa kwenye maji yako ya kunywa ambayo moja kwa moja yataondoa virutubishi visivyofaa katika mwili wako.
PARACHICHI
Lina virutubisho viondoavyo sumu mwilini kama vile carotenoid pamoja na vitamin E.
TIKITI MAJI
Tikiti maji ni tunda muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo wa chakula Kwa kuwa  tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba ambayo husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni.
Kula matunda na mboga za majani ni muhimu sana kwa afya yako kwani ni vitu ambavyo vina utajiri wa vitamini za kutosha lakini pia itakuweka mbali na baadhi ya magonjwa kwani sumu inavyojaa mwilini ndio hivyo magonjwa hayaepukiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni