“Lengo la wimbo huu ni kuwakumbusha na kuwahimiza watu wajiamini wanapofanya jambo lolote jema na lenye kumtukuza Mungu huku wakiwa na mtazamo chanya wa kuona mafanikio mbele yao na kutokata tamaa pale wanapopitia shida kwani shida zinapozidi ushindi unakuwa umekaribia. Watu waamini kuwa vinywa vyao vina nguvu ya kuumba ambapo kama wakivitumia vizuri kwa kujitamkia na kujiumbia mambo mazuri yatakuwa kama yalivyo tamkwa mwisho watu wa Mungu wasitishwe na maadui kwani watakuja kwa njia moja Mungu atawatawanya kwa njia saba wazidi kuona mema mbele yao siku zote.” – alisema Method Mathew
Hakika huu ni moja kati ya nyimbo nzuri ambayo hutakiwi kuacha kusikiliza kila wakati, Huu ni wimbo ambao utakufanya uwe mtu mpya kila siku kwa maana umejaa nguvu ya kukupa mtazamo mpya utaokuwezesha kushinda vita zote mbele yako huku ukimtegemea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika utabarikiwa kila siku, Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni