Breaking

Jumatano, 16 Januari 2019

Video | Eddah Mwampagama – Tumika

Kutoka kwa mtumishi wa Mungu Eddah Mwampagama kwa mara ya kwanza katika mwaka 2019 ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tumika.

Video hii imeongozwa na director Einxer kutoka studio za Muxum Vision, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Mefo Records chini ya mikono ya prodyuza Kingson.
Tumika ni wimbo unaotukumbusha juu ya kumtumikia Mungu maana hiyo ndio maana halisi ya uwepo wetu hapa duniani, Tunakumbushwa kutenda mema kila siku kwa maana nafasi yetu ya kuishi hapa duniani ina mwanzo na mwisho wake, Hakuna ajuaye kesho kwa maana hiyo ni siri ya Mungu peke yake hivyo yakupasa kutumika kwa mambo yatakayompendeza Mungu.
Hii ni moja kati ya video ambazo zitakubariki kila wakati utakapokuwa utazama na kusikiliza, Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na Eddah Mwampagama kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 768 570 055
Facebook: Eddah Mwampagama
Instagram: @eddahmwampagama

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni