Breaking

Jumatano, 9 Januari 2019

Mfahamu Vince Joyn Kutoka Marekani na Huduma Yake Uimbaji

Vince Joyn ni mtumishi wa Mungu ambaye alianza kumwimbia Mungu akiwa katika umri mdogo sana akiwa katika kwaya ya watoto (Sunday school) mkoani Kigoma, nchini Tanzania. Baada ya muda kidogo toka amejiunga na kwaya hiyo aliteuliwa kuwa kiongozi wa kwaya, Na baadae akaendelea kuwa kiongozi hata kwenye kwaya ya vijana na kuendelea.
Mwaka 2008 alihamia nchini Marekani na akaendelea kumwimbia Mungu katika moja ya kwaya iliyofahamika kama Striving for Eternal Life Choir ambapo pia alibarikiwa kuwa kiongozi mkuu wa kwaya hiyo.
Kwa mujibu wa Vince Joyn anasema kuwa kwa muda mrefu amekua na mzigo mkubwa moyoni mwake wa kuipeleka injili kwa njia ya uimbaji na kwamba hata alipokua akiondoka kwenda Marekani, Wachungaji na viongozi wengine wa kanisa walimkumbusha kutoacha kazi hiyo na kile ambacho Mungu alikiongea kuhusu huduma yake.

Mwimbaji Vincent Joyn akiwa nchini Marekani.
“Mara nyingi najikuta nikitokwa na machozi kila ninapokuwa nasikiliza au nikiimba wimbo na ukanigusa, Na ndoto yangu kubwa ni kuona jinsi Mungu atakavyonibariki mimi na huduma yangu ili wengi waokoke na kumtumikia Mungu katika Roho na Kweli.” – alisema
Katika makuzi yangu nilikua napenda sana kusikiliza nyimbo za mwimbaji Yusto (Tanzania), Alexis Dusabe (Rwanda) na Christna Shusho (Tanzania), Kwasasa nasikiliza na ku-support kazi zote za makwaya na waimbaji binafsi na kwakweli nawaombea sana wazidi kusonga mbele katika kazi hii kubwa ya Bwana Mungu wetu.” – aliongeza
Vince ni mume wa mke mmoja wakiwa wamebarikiwa kupata watoto watatu ambao kwa pamoja kama familia wanaishi mjini Des Moines katika jimbo la IOWA nchini Marekani.
Kama bado hujatazama video yake mpya inayokwenda kwa jina la Sifa Zako kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema pia usiache kusubscribe, Ku-Like na kutoa maoni yako pale inapobidi na hakika utabarikiwa, Amen

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Vince Joyn kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 (515) 779-4410
Facebook: Vince Joyn
Instagram: @vincejoyn
Twitter: @vincejoyn
Youtube: Vince Joyn

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni