Breaking

Jumamosi, 5 Januari 2019

Kuna Mambo Mungu Hatafanya Hadi Utoe Sadaka

 
Mwl. Debora E. Lema
UTANGULIZI.

Lazima tuelewe kuwa SADAKA ni kipimo cha upendo kati moyo wa mtu na MUNGU wake.
Kama usivyoweza kujitoa kwa mtu usiyempenda halikadhalika huwezi kujua kumtolea MUNGU kilicho bora kama hujamaanisha kumpenda.

Kumpenda MUNGU si kwa kutamka kwa kinywa, Bali MATENDO uyatendayo ndiyo yatajibu kama unampenda MUNGU au la.

MUNGU anapokuagiza utoe si kwamba ana shida sana na sadaka yako, ila kuna kitu anapima kutoka kwako, pia sadaka huwa inanena yenyewe bila wewe kunena.
MWANZO 15:8-9
“Akasema, Ee BWANA MUNGU, nipataje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwabia, UNIPATIE NDAMA WA MIAKA mitatu, NA MBUZI MKE WA MIAKA mitatu, NA KONDOO MUME WA MIAKA mitatu, NA HUA, NA MWANA NJIWA. (10a) Akampatia hao wote”
MUNGU alimuahidi Abramu baraka. Abramu katika kumuuliza MUNGU ni nani atarithi ikiwa Mimi sina mtoto? Akamuuliza MUNGU ampe udhihirisho ya kuwa atairithi ndipo MUNGU KABLA YA KUMJIBU AKAMWAGIZA KUTOA SADAKA KAMA ILIVYOELEZWA HAPO JUU.
UNIELEWE HIVI, SI KILA JAMBO HUTAJIBIWA MPAKA SADAKA, ILA KUNA BAADHI YA MAMBO ITAKULAZIMU.
MWANZO 22:16b-17
“Wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga uliopo pwani, na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”
KUNA WAKATI MUNGU HAITAJI SADAKA YAKO, ILA ANAPIMA UTAYARI WAKO WA KUMTOLEA.

Ibrahimu hakumzuilia MUNGU mwanae wa PEKEE Isaka. Na baada ya Ibrahimu kwenda na Isaka tayari kwa kumtoa sadaka ndipo BWANA akaachilia mwanakondoo. Kwa moyo wa Ibrahim wa utayari ndipo MUNGU akatamka baraka KUU kwa Ibrahimu kama ilivyoelezwa hapo juu.

KANUNI ZA UCHUMI WA KIDUNIA NI KUZUIA MILANGO WA KUTOA FEDHA NA KUFUNGUA MILANGO YA KUINGIZA FEDHA, LAKINI KANUNI YA KIMUNGU NI KUACHILIA MLANGO WA KUTOA NDIPO UPOKEE.
MUNGU AKUBARIKI, CHUKUA KILICHO CHEMA NA UKITENDE KWA UTUKUFU WA BWANA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni