ANDIKO KUU: WAEFESO 6:12
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, Bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya Wakuu wa Giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya *KATIKA ULIMWENGU WA ROHO”
UTANGULIZI
Neno la Mungu linatutaka kupigana vita vya kiroho, na Wala si juu ya damu na nyama. Kwa maana hiyo katika SOMO HILI LAZIMA TUJUE ulimwengu wa roho ni upi huo? Na Vita yake ipoje? Na watu gani wenye sifa ya kupigana vita hyo?Silaha katika Vita hiyo ni nini? Utafanyaje kushinda Vita hiyo? Kwa nini wengi wanashindwa Vita hiyo? Na mambo kadha wa kadha yafananayo na hayo. “TUNAYE MWALIMU AMBAE NI ROHO MTAKATIFU ATAKAE TUFUNDISHA PAMOJA”
Tukirejea andiko letu kwamba kupigana kwetu si kwa damu na nyama, Bali katika ULIMWENGU WA ROHO (Waefeso 6:12).
Zipo maana nyingi sahihi na nzuri kuhusu ulimwengu wa Roho. Lakini mimi naweza kusema ulimwengu wa roho ni Ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama, ambapo mtenda kazi mkuu anaweza kuwa Mungu au Shetani
Mambo yanayotokea katika ulimwenguu huu tunaoushuhudia kwa macho ya damu na nyama huwa ni kivuli cha ULIMWENGU WA ROHO.Kwa maana kwamba yalishatendeka ila udhihirisho Ndio unajitokeza Baadae katika ulimwengu kivuli.Yapo mandiko mengi yanayoweza kukupa mwangaza. Tutazame Yeremia 1:5
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa ”
Pia tuone Isaya 46:10
“Nitangazae mwisho tangu mwanzo……..
Hapo kwa Yeremia 1:4..maneno Mungu alimwambia, Jeremiah, unaweza ona katika ulimwengu wa Roho tayari Mungu alishajua Jeremiah atazaliwa, na atakua nabii wa mataifa.
Hii inamaana kuwa hata wewe Mungu anakujua wewe baada ya miaka kadhaa utakua wapi, utakua nani, bila kujali mazingira unayopitia au uliyopo.
Shetani nae anakuwinda vile vile, na Dalili za mawindo yake huwa ni dhahiri, nitazielezea tunavyoendelea pia.
JE, WEWE UNAWEZA KUUMBA KITU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NA KIKAWA DHAHIRI?
JIBU NI NDIO.
TUSOME AYUBU 22:28
” Nawe UTAKUSUDIA neno, nalo LITATHIBITIKA kwako, na mwanga utaziangazia njia zako ”
Watu wa Mungu huwa TUNAKUSUDIA*na *KUUMBA*Mambo katika ulimwengu wa *ROHO.Neno la Mungu linatupa uhakika kuwa sisi kama wana wa Mungu (Si watoto, wana) kuwa tunaposhiriki kuumba au kukusudia mambo katika ulimwengu wa Roho, *YATATHIBITIKA*Kwa maana tutayaona katika ulimwengu kivuli, yaani ulimwengu wa Damu na Nyama.
Mambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa damu na nyama tayari yalikwisha ratibiwa rohoni. Hivyo anza kukusudia mambo rohoni kusudi yanayotokea uwe tayari ulishayajua. Si kila jambo kwako liwe jipya, mengine uwe tayari ulishayajua Kwa maana ya kuyaona yatakavyokua
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni