Mkali wa sauti akiwa moja kati ya waimbaji wanaoendelea kufanya vizuri katika huduma ya muziki wa Injili Tanzania huyu si mwingine bali ni Eliud Martine ambaye leo hii ametusogezea wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nitakaa Nawe.
“Nitakaa Nawe Ni wimbo ambao unaelezea ni jinsi gani Mungu anafanya kazi kubwa katika maisha yetu ya kimwili na roho hadi tunapata shauku ya kutaka kujifunza kutoka kwake ili tuwe na moyo wa ukarimu kama yeye, upendo usio na kikomo.
Msukumo huu unafanya wakristo wengi kufurahishwa na makuu yake Mungu na kutaka #KUKAA NAYE KARIBU ILI KUZIDI KUJIFUNZA MENGI. *USHAURI* MUNGU KWETU NDIYE KIMBILIO NA WAMWABUDUO KATIKA KWELI NAO WATA MUONA #TAMANI KUKAA KARIBU NA MUNGU UJIFUNZE MENGI.” – alisema Eliud
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri ambao ni hakika utakubariki kila wakati, Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni