Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Atupele Alfred amefunguka juu ya kuachia rasmi albamu yake mpya inayobebwa na jina la Mungu Umetamalaki, ikiwa ni albamu yake ya kwanza kuachia toka aanze huduma ya uimbaji miaka kadhaa iliyopita.
Albamu hii ina mkusanyiko wa nyimbo nane katika mfumo wa Audio CD zote zikiwa zimefanyika ndani ya studio za Ngomale Records chini ya mikono ya prodyuza Daniel Kajinga akishirikiana na Agape Kapesa.
Mwimbaji Atupele anasema:
“Album nzima ina nyimbo tofauti tofauti ambazo kwa pamoja zina lengo moja tu la kueneza Injili, Mungu umetamalaki ndio jina la albamu hii ukiwa ni wimbo pekee unaoeleza jinsi Mungu alivyo kila mahali.
Na kwa ujumla albamu nzima inaongelea uweza wa Mungu na upendo wa Mungu kwetu na ikimsifia Mungu kuwa hakuna mwingine kama yeye maana ana uwezo mkubwa na anatupa baraka kila iitwapo leo.” – alisema
Hii ni moja kati ya albamu ambazo hutakiwi kukosa kuipata nakala yako kwakua ni albamu iliyobeba ujumbe wa Ki-Mungu utaobadilisha maisha yako kiroho na kimwili.
Kwa mawasiliano zaidi juu ya jinsi ya kuipata nakala ya albamu hii, mialiko ya kihuduma tafadhali wasiliana na mwimbaji Atupele Alfred kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 655 535 115
Facebook: Atupele Alfred
Instagram: @atupelealfred
Simu/WhatsApp: +255 655 535 115
Facebook: Atupele Alfred
Instagram: @atupelealfred
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni