Hivi karibuni kumekuwa na msako
mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China
uliosababisha taharuki kubwa kwamba serikali ya nchi hiyo inaonesha
ubabe wake wa
kuwakandamiza Wakristo.Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi mmoja maarufu pamoja na mkewe. Wote ni wamiliki wa kanisa la Early Rain Covenant lililoko katika jimbo la Sichuan. Wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la kuhujumu utendakazi wa serikali ya kikomunisti ya China na kwenda kinyume na maadili ya Wachina.
Jumamosi asubuhi, kikosi cha polisi kilivamia darasa moja la kidini lililokuwa likiwapa mafunzo watoto ndani ya kanisa la Rongguili huko Guangzhou.
China ni nchi isiyomuamini Mungu, japo mamlaka zinasema zinatoa uhuru wa kuabudu.
Lakini kwa miaka mingi utawala wa nchi hiyo umechukua hatua dhidi ya viongozi wa kidini, ambao wanaonekana kutishia mamlaka au kuyumbisha uongozi wa taifa.
Serikali inawashinikiza wakristo kujiunga na mojawapo ya makanisa makubwa matatu yanayoonyesha uzalendo kwani zimepigwa msasa na serikali pamoja na chama tawala cha Kikomunisti, huku yakiongozwa na makasisi walioidhinishwa na serikali.
Licha ya haya, idadi ya wakristo inaoongezeka kila uchao hasa katika miaka ya hivi karibuni. Mpaka kufikia sasa inakadiriwa kuwa China ina zaidi ya wakristo milioni 100, wengi wao wakiabudu ndani ya makanisa yaliyoko katika vyumba vya chini kwa chini.
Chanzo: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni