Akiongea na Gospomedia.com Frank Mathew amesema kuwa Tour hii ya Comedy itafanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Dodoma, Dar es salaam na mikoa mingine.
“Mnamo tarehe moja ya mwezi Januari 2019 show hii ya Comedy inatarajiwa kuanza kuvunja mbavu wa wakazi wa Arusha ndani ya ukumbi wa Hoteli ya kimataifa pale Arusha mjini ijulikanayo kama Corridor Spring Hotel, kwa Kiingilio cha Shilingi 20,000 VIP, 10,000 kawaida na 5,000 kwa watoto….” – alisema
Mbali na mchekeshaji Frank Mathew, Watakuwepo wachekeshaji wengine kutoka mikoa mbalimbali na nje ya Nchi ya Tanzania kama vile Mc Willy kutoka Dar es salaam, Mkibosho kutoka Kilimanjaro, Dr Kitenge kutoka Morogoro na na wengine wengi toka Arusha, n.k.
“Event inatarajiwa kuanza mnamo majira ya saa tisa jioni mpaka saa moja jioni, Wakazi wote wa kaskazini mnakaribishwa sana katika tukio hili kubwa mno kuwahi kutokea Jijini Arusha.” – alimaliza
Kwa mawasiliano zaidi tembelea ukurasa wao wa Instagram @cheka.tena ama tuma ujumbe mfupi kupitia simu namba +255 759 357 393, Cheka Tena Arushaaaaa, Tunacheka kikwetu kwetu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni