Breaking

Ijumaa, 5 Machi 2021

UNAFANYA NINI BAADA YA KUSIKIA?


 

Bwana YESU  asifiwe.Ninakukaribisha tena leo tujifunze somo lenye kichwa cha habari kinachosema,UNAFANYA NINI BAADA YA KUSIKIA?

❖ Sote tunajua kuwa Imani chanzo chake ni kusikia sawa na maandiko kutoka kitabu cha warumi 10:17( Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo)kwa hiyo basi habari unayoisikia ndiyo inayoleta Imani kwako.

❖ Maamuzi yako baada ya kusikia yanaweza kukufanya ukabaki hapo hapo ulipo,ukarudi nyuma au ukasonga mbele.Si kila jambo unalosikia ni la kufanyia kazi,mambo mengine ukisikia unatakiwa uyaache kama yalivyo na habari nyingine ukisikia ni za kuzifanyia kazi.Shetani hutumia watu kukuletea habari mbaya kwako za kukukatisha tamaa,kukurudisha nyuma na kukufanya ushindwe kujiamini.Lakini pia hata mazingira yanayokuzunguka yanaweza kuleta  sauti ndani ya akili yako ambayo ikaleta hofu na mashaka na kukurudisha nyuma.

❖ Habari mbaya za kukatisha tamaa zikija kwako hupaswi kuziweka akili mwako na kuziamini kwa sababu zimekuja kwa kusudi la kukuangusha.watu wanaweza kuja kwako na kukuambia kuwa huwezi kufanikiwa,wengine watasema huwezi kupata kazi,wengine watasema huwezi kuoa au kuolewa,wengine watasema kuwa umelaaniwa,wengine watasema kuwa huna akili.swali linakuja je wakikuambia hivyo unafanya nini?utawaamini na kuanza kuogopa,utapuuza maneno yao na kusonga mbele au utabaki tu ukilia na ukiona kuwa basi imekwisha.

❖ 1samweli 17;10-11 ( Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane.Basi Sauli na Israeli wote waliposikia maneno hayo ya Mfilisti, wakafadhaika na kuogopa sana)Ukisoma habari hizi utaona kuwa kilichowafanya waisraeli kufadhaika na kuogopa ni baada ya kusikia vitisho kutoka kwa Goliati.lakini sio kwamba waisrael walikuwa hawawezi kumpiga Goliati ,walikuwa na uwezo huo kwa kuwa Mungu aliwaahidi kuwa atakuwa nao siku zote.

❖ Ukisoma sura hiyo mstari wa 24 ..( Na watu wote wa Israeli walipomwona yule mtu wakakimbia, wakaogopa sana.)hapa utaona kuwa baada ya kuingiwa na hofu wakachukua hatua ya kumkimbia)

❖ Unatakiwa ujiamini pale unapokuwa  Na Mungu, habari mbaya ikija kwako isikufanye ukapoteza tumaini.Unamchukuliaje Mungu unayemuabudu?kwani kuna Neno la Kumshinda Mungu?

❖ 1samweli17:32 (Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.).Ikija habari mbaya kwako ya kukutia hofu unapaswa kusimama imara wala usizimie Moyo

 

Yote yanawezekana kwako Mtumishi wa Mungu maana Mungu ndiye anayekutia nguvu siku zote.

 

Mungu akubariki sana

 

Apostle Daniel

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni