Breaking

Jumanne, 2 Machi 2021

Mungu Yupo Nawe Katika Njia Unayopitia

 




Bwana Yesu asifiwe


Mathayo 16

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.


23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu


Ukisoma hayo maandiko utaona kuwa Bwana Yesu alijua kuwa lazima apitie mateso ili afe halafu afufuke ndipo apate ushindi na ndipo mimi na wewe tufanyike kuwa wafalme Lakini Petro alimwambia Yesu kuwa hayo hayatompata.Kwa hiyo tunajifunza kuwa wengine ili wainuliwe ni lazima wapitie mateso kwanza ndipo wawe katika viwango vipya na waingie katika msimu mpya wa mafanikio.kwa hiyo shetan anaweza akamtumia mtu ukaona kuwa anakupa msaada lakini kumbe anafanyika kikwazo kwako usiende mbele.mwingine anaweza kuja kwa lengo la kukupa ushauri mbaya,mwingine anaweza kukwambia kuwa wokovu hauna faida yoyote,kuwa makini sana na watu wanaokuja kwako ukiwa unapita kwenye hali ngumu ya maisha.


Mtumishi wa Mungu unatakiwa ujue kuwa kila mtu ana njia yake ya mafanikio.kuna wengine njia zao ni moto,wengine njia zao ni mito ya maji,wengine katika njia zao kuna ukuta.kwa hiyo ili wafanikiwe lazima wapite katika njia hizo ngumu.Na kama wakiamua kutafuta njia zenye wepesi kamwe hawatoshinda watabaki palepale.


Njia ya kumpa ushindi Bwana Yesu ilikuwa ni mateso,kuaibika,kudharauliwa,kutemewa mate.lakini ndio njia aliyoandaliwa ili tupate ushindi ✳️Ufunuo 2:10

10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


ukisoma hayo maandiko utaona kuwa kuna wengine ni lazima wapite kwenye gereza la mateso maana ndio njia yao ya kuinuliwa.maandiko yanasema tuwe waaminifu hata kufa,maana yake tusikate tamaa hata kama kila kitu kikiharibika.


Unajua ukiwa mtu wa mwilini huwezi kumpendeza Mungu kwa sababu miili yetu inataka tumkosee Mungu.ili uwe mshindi unatakiwa roho yako iwe na nguvu kuliko mwili wako.kwa hiyo Mungu anataka tuwe waaminifu hata mauti anamaanisha kuwa tufikie mahala miili yetu isitudanganye,tufike mahala miili yetu isituambie turudi nyuma,ifike mahala miili yetu isituambie tumuache Mungu eti kisa 

changamoto.mwili wako unapokufa na roho yako ikajawa na Roho mtakatifu ukaweza kuushinda mwili ndipo utakapouona utukufu wa Mungu 

Yusuphu ilikuwa lazima apitie gerezani ili aje kuwa mkuu katika nchi ya misri.kama asingepitia gereza maana yake asingekuwa mkuu,kwa hiyo kama ningekuwepo kipindi kile na kumkataza asiingie gerezani maana yake ningekuwa nataka Yusuphu asiwe mkuu

 Ifikie kipindi mwambie Mungu kuwa "hata kama nipo gerezani Baba sitokuacha,mwambie Mungu kuwa hata kama napitia mateso sitokuacha"

Songa mbele mtumishi wa Mungu,utashinda hata kama unapitia moto ✳️Isaya 43:2

2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza

 Kama wewe njia yako ni kwenye maji Mengi Mungu yupo nawe 

kama njia yako ni kwenye mito haitakugharikisha

 kama njia yako ni kwenye moto hautateketea 

na kama unapita kwenye mwali wa moto hautokuunguza 


✳️kila njia upitayo Mungu yupo na wewe✳️


          Mungu akubariki sana 


                        Apostle Daniel


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni