Breaking

Alhamisi, 11 Machi 2021

MSAMAHA



 Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.Siku ya leo tutazungumzia Msamaha
✅msamaha au kumsamehe mtu limekuwa ni jambo gumu sana kufanywa na wanadamu.Watu wengi wanashindwa kusamehe pale ambapo wametendewa mambo magumu na ya kuumiza sana.kutokusamehe huku kumesababisha watu kutembea na maumivu makubwa ndani ya  mioyo yao,na maumivu haya yamesababisha watu wengine kupata magonjwa kama vile pressure.Kutokusamehe huku kunafungua mlango wa mauti unaoweza kukuletea kifo,lakini pia kutokusamehe ni kifungo cha ibilisi.
✅Tabia ya Mungu ni kutusamehe na ndio maana hata umkosee mara ngapi Mungu ni lazima atakusamehe na tena anasahau kabisa makosa uliyomkosea.Kwa hiyo kama sisi tumeokoka tunapaswa kusamehe kwa sababu Bwana Yesu tulie naye mioyoni mwetu ni wa msamaha,na kama hatusamehi maana yake kuokoka kwetu na ukristo wetu ni bure.kipimo cha mkristo ni upendo na ndani ya pendo kuna msamaha.
⏺Marko11:25-26
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
✅maandiko yanasema kuwa kila tusimamapo kusali tusamehe,kwa hiyo kama hujasamehe maana sala zako unazofanya ni bure na maombi yako hayafiki popote maana yanazuiliwa na hali ya kutokusamehe.
⏺ 1Yohana 2:11
11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
✅Usiposamehe unasababisha chuki kuingia ndani yako na chuki ikiingia ndani yako inakaribisha giza maishani mwako na lolote utakalofanya litashindikana kwa sababu ya hilo giza
✅Wengine wamekuwa  wanaishi maisha ya mateso kwa sababu tu ya kutokisamehe
✅Silaha ya kusamehe ni kutokuhesabu mabaya.ukiwa mwepesi wa kusahau mabaya na kukumbuka mazuri ya mtu utakuwa mwepesi sana kusamehe
✅Nina imani kuwa huyo aliyekukosea yapo mazuri hata machache aliwahi kukufanyia basi kumbuka hayo mazuri tu na usikumbuke mabaya.Kumbuka hata Mungu mwenyewe hakumbuki mabaya ambayo wewe na mimi tunamkosea sasa kwa nini wewe ni mwepesi kukumbushia mabaya uliyofanyiwa?
✅Utajuaje umeweza kumsamehe mtu
1.Ukimuona huyo aliyekukosea unaona upendo kwako juu yake
✅ukimuona aliyekukosea moyoni mwako hakujai hasira wala kumchukia
Mungu akubariki sana amua siku ya leo kusamehe wote waliokukosea ili ufungulie baraka za Mungu juu yako.
Apostle Daniel(whatsapp 0756277095)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni