Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu.leo nitasema na wewe Neno la Mungu lenye kichwa kinachosema(hakuna jambo gumu lisilo na mwisho)
✳️Katika maisha tunayoishi wapo watu ambao wanapitia changamoto mbali mbali,wapo ambao wamekata tamaa na kurudi nyuma,wapo ambao bado wanasonga mbele na wapo ambao wameshindwa na kuamua kurudi nyuma.
✳️Mungu anajifunua kuwa yeye ni Alfa na Omega(Mwanzo na Mwisho)akimaanisha kuwa yeye anajua mwanzo wetu na anajua mwisho wetu.Yeye Mungu yupo nasi katika kipindi chote tunachopitia
✅Kwa hiyo basi lazima uelewe kuwa hakuna mateso yasiyo na kikomo,Mungu hawezi kuruhusu upitie shida na mateso siku zote kwa kuwa yeye Mungu ni pendo.
✅Kumb 2:3
3 Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini.Maandiko hayo yanaonesha kuwa waisrael walitumia mda mwingi kuzunguka milima ya Seiri lakini wakati wao ulifika na Mungu akawaambia kuwa imetosha kuzunga katika mlima huo.
✅Wewe unayesoma ujumbe huu nakuambia kuwa kuna wakati wako ambao utafika ambapo hutopata mateso uliyopata awali bali Mungu atakukumbuka na kukuinua
✅Kuna ambao wanafikiri kuwa Mungu amewaacha eti kwa sababu wanapitia mateso makubwa yasiyoisha.Mungu hawezi kukuacha na ameahidi kuwa hatokuacha
✅Wakati wako unakwenda kufika ambapo Mungu atakufuta machozi,Mungu anakwenda kuondoa aibu yako,Mungu anakwenda kukuheshimisha ple ulipodharauliwa.
Mungu akubariki sana
Apostle Daniel
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni