Breaking

Jumamosi, 16 Mei 2020

Mambo Tusiyopenda Lakini Yenye Mchango Mkubwa Katika Kustawi Kwetu ( Sehemu 1)

Mwalimu Deborah E. Lema
  1. WAKATI WA KUSUBIRI.
Ni wakati ambao watu wengi hawaupendi. Kila mmoja anapenda kusikia kuwa huu ni wakati wako wa kubarikiwa, huu ni wakati wako wa kuvuna, huu ni wakati wako wa kumiliki na kutawala, na jumla ya mambo mengi mazuri ya kupendeza masikioni mwetu. Yawezekana uliambiwa mwaka huu ni mwaka wako wa kufanya mambo makubwa, lakini yamkini kwa mujibu wa kalenda ya Mungu huu ni mwaka wako wa kwanza kati ya ile mitano aliyopanga Mungu kwa ajili ya kukuandaa kwa ajili ya jambo Fulani.

Haijalishi hii ni habari mbaya masikioni mwako, lakini kama Bwana amekusudia hivyo itakua tu. Huwezi ukapenda kuvuna kila wakati tu, kuna wakati wa kupanda, utapalilia ndipo uje uvune. Na wakati mwingine pia wadudu wanaweza haribu shambani kwako itakubidi uanze upya. Na wadudu wanapoharibu sio kwamba Mungu anashindwa kuwazuia HAPANA. Kwani hujasoma habari za Musa na Farao? Kwamba Mungu huyo huyo anayemtuma Musa kwa Farao ndio Mungu huyo huyo anaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu?
Hujasoma habari za Ibrahimu katika MWANZO 15:4-7 vile ambavyo BWANA alimuahidi Ibrahimu baraka nyingi? Unadhani zilitimia juma lililofuata? Kama alimsubirisha Ibrahimu, unadhani kwako atashindwa?
Na usijaribu kumziria Mungu au utafute njia ya mkato, yamkini jibu lako lipo mwaka wa kumi na huu ni mwaka wa 9, maamuzi yako yasiyo na ufahamu wa rohoni yanaweza kukufanya ukaanza mwaka wa kwanza mwakani usubiri mingine tisa mbeleni. USICHOKE KUSUBIRI.



2. KUKATALIWA.
Unataka kila mtu akubaliane na mawazo yako, akubaliane na huduma yako, kazi yako, biashara yako n.k Ni jambo zuri sana, lakini unakumbuka mambo mazuri aliyoyafanya Yesu lakini bado wakamdhihaki na kumsema vibaya? Unadhani kuna mambo mazuri unayoweza kufanya Zaidi yake ili kila mtu akuunge mkono wa shirika?
Wengi wamerudi nyuma na kuacha kutimiza malengo yao ukiwauliza wanasema ndugu waliwatenga, au marafiki waliwasema vibaya. Ni bora wakubaliane na upotovu wako au ni bora wakukatae lakini uwe kwenye njia sahihi? Mambo mangapi ulighairi kufanya kwa sababu watu hawakukuonyesha ushirikiano? Au walikupa muitikio mdogo tofauti na ulivyotegemea? Unakumbuka maneno ya wale waliomdhihaki YESU baada kifo chake? MATHAYO 27:54 Neno linasema
Basi yule akida, na hao waliokua pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la nchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, HAKIKA huyu alikua Mwana wa Mungu.
Hakuna mtu aliyewalazimisha wasadiki, ila wakati ulipofika wenyewe kwa vinywa vyao walikiri bila kulazimishwa na mtu. Nikushauri jambo moja mtu wa Mungu, usitumie nguvu kubwa na muda wako mwingi kuwalazimisha watu wakukubali. Huo muda na hizo nguvu zitumie kufanya kile ambacho ni sahihi, muda utafika watakuja kwa aibu mbele zako au watashuhudia kwa mbali matunda yako. MAADAMU BWANA AMEKURIDHIA, WEWE FANYA KWA BIDII NA KWA UAMINIFU.
Hakuna mtu aliyewalazimisha wasadiki, ila wakati ulipofika wenyewe kwa vinywa vyao walikiri bila kulazimishwa na mtu. Nikushauri jambo moja mtu wa Mungu, usitumie nguvu kubwa na muda wako mwingi kuwalazimisha watu wakukubali. Huo muda na hizo nguvu zitumie kufanya kile ambacho ni sahihi, muda utafika watakuja kwa aibu mbele zako au watashuhudia kwa mbali matunda yako. MAADAMU BWANA AMEKURIDHIA, WEWE FANYA KWA BIDII NA KWA UAMINIFU.



3. MWANZO MDOGO.
Tatizo la watu wengi wanapenda matokeo makubwa lakini hawaukubali mchakato wa kuyafikia hayo matokeo makubwa. Mtu anataka aanze moja leo kesho awe kwenye mia.
Wengine wamekosa na uaminifu katika hayo madogo wakidhani ya kuwa wakishafika kwenye viwango vya juu wataweza kuwa waaminifu. Neno halijatuficha katika hilo, LUKA 16:10 inasema
“Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.”
Mungu anapotaka kukufikisha mahali pa juu, kuna mahali atakupitisha kama majaribio ya kukupima baadhi ya vitu. Atapima utii wako, nidhamu yako, uaminifu, bidi n.k Unadhani kwanini yule mwana mpotevu aliyeomba sehemu ya urithi kwa baba yake hakuweza kudumu na zile mali? Alipata vitu vingi ambavyo hakuvitolea jacho wala kulipa gharama, hivyo akavitumia ovyo ovyo (LUKA 15:11-32). Usiudharau huo mwanzo mdogo, Haijalishi ni huduma, ni ndoa, ni kazi, ni biashara n.k Fanya kwa bidi na kwa uaminifu huku ukimtanguliza Mungu mbele.
4. KUSHUGHULISHWA NA MAMBO MANYONGE.
Watu wengi huchelewa kufikia hatima zao au hata kutokuzifikia kabisa kwa sababu kuna mambo wanayadharau na kuyaona ni upuuzi au yakishamba kwamba hawastahili kuyafanya. Unakuta kama ni mtumishi anataka moja kwa moja aanze kuheshimika, kufahamika na kupewa sifa kebekebe. Mtu analalamika hana cha kufanya kikamgusa Mungu, ukimuuliza kanisani kwenu huwezi kufuta viti? Au hata kufanya usafi? Utamsikia sasa kazi gani hiyo? Si bora nikae nyumbani tu? Hayo yote ni kwa sababu watu hawako tayari kuyinyenyekesha BWANA awakweze kwa wakati wake. (1 PETRO 5:6)
Tamani MUNGU akukweze kwa wakati wake. Fanya yale mambo ambayo yanadharaulika na kuonekana hayana maana. Wale wahitaji na masikini waliotelekezwa jitoe kwa ajili yao, usiwe mtu wa kufanya mambo ambayo utaonekana na watu wakusifie. Fanya ili BWANA akuone, thawabu yako ipo juu kwa Baba. Huwezi kusema umekosa kitu cha kufanya ambacho kitampa Mungu utukufu. Tatizo tunataka mambo makubwa ambayo si ya kujitaabisha. Neno linasema katika WARUMI 12:16 ya kuwa
“…Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.”
Je, ni kweli unakubali kushughulishwa na mambo manyonge? Ni kweli kuna wakati unaweka cheo chako pembeni, pesa na umaarufu na kujishusha chini kwa ajili ya utukufu wa Mungu? KUFANYA MAMBO MANYONGE HAKUSHUSHI THAMANI YAKO MBELE ZA MUNGU.


Maonyo

5. KUKEMEWA NA KUONYWA.
Tumekua watu wa kupenda sifa na kukataa kuambiwa ukweli ambao ungetufikisha mahali fulani pazuri. Tumekua watu ambao hata tukikosea tunataka tusifiwe na kupambwa kwa maneno mengi ya unafiki. Watu hawataki kukemewa kuhusu maadili wanataka wapewe uhuru uliopitiliza wa kujiamulia wanavyotaka. Neno la Mungu katika 1 Wathesalonike 5:14 linasema;
“Ndugu, twawasihi, WAONYENI wale wasiokaa kwa utaratibu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.”
Msisitizo wangu upo hapo katika kuonya wasiokaa katika utaratibu. Kila jambo lina utaratibu wake. Hivyo tegemea unapokosea uonywe unaposhupaza shingo ukemewe.
Na! Kuambiwa ukweli unapokosea sio kuhukumiwa, kuna watu wanatabia wakiambiwa ukweli wanasema wanahukumiwa (UKWELI SI HUKUMU).
Itaendelea…


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni