
Hivi karibuni kumekuwa na msako
mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China
uliosababisha taharuki kubwa kwamba serikali ya nchi hiyo inaonesha
ubabe wake wa
kuwakandamiza Wakristo.Miongoni mwa waliokamatwa ni kasisi mmoja maarufu pamoja na mkewe. Wote ni wamiliki wa kanisa la Early Rain Covenant lililoko katika jimbo la Sichuan. Wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la kuhujumu utendakazi wa serikali ya kikomunisti ya China na kwenda kinyume na maadili ya Wachina.
Jumamosi asubuhi, kikosi cha polisi kilivamia darasa moja la kidini lililokuwa likiwapa mafunzo watoto ndani ya kanisa la Rongguili huko Guangzhou.

Kanisa la Early Rain Covenant, limeweka picha hii ya maombi yao katika mtandao wa kijamii wa Facebook
Lakini kwa miaka mingi utawala wa nchi hiyo umechukua hatua dhidi ya viongozi wa kidini, ambao wanaonekana kutishia mamlaka au kuyumbisha uongozi wa taifa.
Serikali inawashinikiza wakristo kujiunga na mojawapo ya makanisa makubwa matatu yanayoonyesha uzalendo kwani zimepigwa msasa na serikali pamoja na chama tawala cha Kikomunisti, huku yakiongozwa na makasisi walioidhinishwa na serikali.

Wang Yi ni kiongozi maarufu wa kanisa moja lisilo rasmi nchini China
Chanzo: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni